Pages

Thursday, May 17, 2012

Ajali iliyotokea jana Singida



Singida
WATU wane wamelazwa hospitali ya Mkoa Singida, baada ya basi la Mohamed Trans, kugongana na basi dogo, mjini Singida.
Kamanda wa Polisi mkoa Singida, Celina Kaluba, amesema chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva basi la Mohamed Trans, aliyejaribu kuingia katika barabara kuu ya Mwanza- Dodoma, bila kuchukua tahadhari yoyote.Hata hivyo dereva wa basi la Mohamed Trans ambaye jina lake halikupatikana, alitoroka.
Majeruhi waliolazwa ni Yesaya Samson(dereva wa basi dogo) aliyevunjika miguu yote, Paulo Rajabu, Parick Stephano na William Richard, waliopata majeraha sehemu mbalimbali za miili yao.
Abiria zaidi ya 50 waliokuwa kwenye basi la Mohamed Trans hawakupata madhara, huku wenzao wanne wa waliojeruhiwa na kulazwa walikuwa abiria wa basi dogo.
Ajali hiyo imehusisha basi namba T 848 BEQ Scania, kampuni ya Mohamed Trans likitoka Morogoro kwenda Mwanza na basi lingine dogo namba T 499 BRS Dyana, likitokea Singida mjini, kwenda kijiji cha Iglansoni, Singida vijijini.
Kutokana na ajali hiyo, Kaluba amewakumbusha madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani, ili kuepusha ajali zisizokuwa za lazima.

No comments:

Post a Comment