Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, May 24, 2012

ANGALIA HAPA JINSI WANANCHI WA MALI WALIVYOVAMIA IKULU NA KUMPIGA RAIS.

.
Baada ya kumpiga rais wa nchi hiyo, wananchi wakawa wamepumzika hapo hapo Ikulu.
.
Hizi picha ni wakati waandamanaji wenye hasira walipovamia na kumpiga Rais wa muda wa Mali Diancounda Traore juzi ambapo ilikua kama mzaha, waandamanaji hao waliokua na hasira walivamia Ikulu ya nchi hiyo na kumpa kipigo rais huyo huku walinzi wake wakitizama, hasira za raia hao zilisababishwa na kitendo cha Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magahribi, ECOWAS kumlaazimisha kiongozi wa mapinduzi ya Machi 22 Kapteni Amadou Sanogo akubali kuongeza muda wa serikali ya mpito inyoongozwa na rais Traore kwa miezi kumi na mbili.
Msemaji wa wanajeshi waliyofanya mapinduzi hayo Bakary Mariko, alisema walinzi wa rais Traore waliua watu watatu katika uvamizi huo japo taarifa nyingine zinasema walinzi hao walikaa na kutizimana huku wananchi hao wakijivinjari katika viwanja vya Ikulu, huku wengine wakionekana kuegesha pikipiki na baiskeli zao katika eneo la  ikulu na kuchana picha za rais Traore.

No comments:

Post a Comment