Pages

Monday, May 7, 2012

ANGALIA HAPA MATUKIO YA PICHA ZA KUAPISHWA MAWAZIRI WAPYA



 Rais Dk. Jakaya Kikwete akiwa katika viwanja vya Ikulu leo mara baada ya kumaliza kazi ya kuwaapisha mawaziri na manaibu waziri wapya aliowateua hivi karibuni, Fullshangweblog Ikishuhudia tukio hilo kwenye viwanja vya Ikulu  leo sasa  inakumuvuzishia matukio mengine mbalimbali yaliyojitokeza katika hafla hiyo iliyofanyika Ikulu  jijini Dar es salaam.
 Naibu waziri wa Sayansi na Teknolojia January Makamba akihojiwa na mtangazaji wa BBC mara baada ya kuapishwa leo.
 Rais Dk Jakaya Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Said Mwema.
 Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na mmoja wa watoto walliohudhuria na wageni mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo ya kuapishwa kwa mawaziri
 Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Majeshi nchini Jenerari Davis Mwamunyange kushoto ni Waziri wa Ulinzi Shamsi Vuai Nahodha
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk Fenela Mukangara akila kiapo mbele ya Rais Jakaya Kikwete leo.
 Naibu waziri wa Sayansi na Teknolojia January Makamba akila kiapo.
 Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Angela Kairuki akila kiapo
 Mwandishi wandamizi wa Magazeti ya Mwananchi Communication Bathoromeo Mkinga akisaidia mzee Sabodo kuelekea katika eneo la kukaa wageni waalikwa, kushoto ni Waziri wa Wanawake Jinsia na Watoto Mh. Sophia Simba.
Ridhiwan Kikwete akizungumza na aliyekuwa rais wa Yanga Jamal Malinzi wakati wa hafla hiyo katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam leo.
 Miraji Kikwete akiwa na wadau wengine katika hafla hiyo
 Rais Jakaya Kikwete akipiga picha ya pamoja na mawaziri pamoja na manaibu waziri mara baada ya kuwaapisha leo.
 Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na manaibu Waziri mara baada ya kuwaapisha leo Ikulu

No comments:

Post a Comment