Pages

Tuesday, May 8, 2012

POLISI YAMSAKA MBUNGE WA ARUMERU MASHARIKI



Na Gladness Mushi wa Fullshangwe-Arusha
JESHI  la Polisi limempa masaa machache Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Bw Joshua Nassari na endapo kama hatajisalimisha kwa jeshi hilo basi nguvu  zaidi zitatumika katika kumsaka kwa kuwa Mbunge huyo ametoa lugha za uchochezi kwa wananchi juzi katika mkutano ambao ulihudhuriwa na viongozi wa juu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)
Hayo yalisemwa na Naibu Kamishna wa jeshi la Polisi hapa nchini Bw Isaya Mngulu wakati akiongea na vyombo vya habari mapema jana jijini hapa
Kamanda Mngulu alisema kuwa Mbunge huyo alitoa matamko hayo katika viwanja vya NMC  juzi ambapo alidai kuwa Rais hapaswi kufika katika kanda ya kaskazini hasa katika jimbo hilo endapo kama atashindwa kufuatilia sakata la mauaji  ya aliyekuwa kada wa  Chadema kwa haraka sana
Aidha aliongeza kuwa  mbali na mbunge huyo kusema maneno hayo pia aliwaambia wananchi waliokuwa umati mkubwa sana katika maeneo ya viwanja vya NMC kuwa  yeye ndiye atakayekuwa Rais  wakati  Waziri mkuu atakuwa ni Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini Bw Goodbless Lema hali ambayo inaonesha kauli za uchochezi
“Hizi kauli ni za uchochezi mkubwa sana na tumejaribu kumtafuta kwa kila njia lakini hajaonekana na sasa tunatumia vyombo vya habari kumtafuta na endapo kama hatajitokeza tutatumia mbinu za kijeshi kumsaka ili ajibu alichokikiri”alisema Bw Mngulu
Akiongelea sakata la baadhi ya wanachama wa Chadema kudai kuwa wanatishiwa kuwawa na watu wasiojulikana kuwa madai hayo ni ya uongo na wanaotuma na kusambaza ujumbe mfupi(SMS) ni  makada wa Chadema na mpaka sasa Jeshi hilo limeshawabini
“ninachotaka kuwaambia ni kuwa hawa watu wa Chadema wanatakiwa kujua sisin Polisi sio watoto wadogo wa kudanganywa tulichokijua ni kuwa wanatumiana SMS wao wenyewe  na tunafanya upelelezi na tutahakikisha kuwa tunawatia Mbaroni”alisema Bw Mngulu
Awali alisema kuwa mpaka sasa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limefanikiwa sana kuwatia Mbaroni watu12 ambao walihusika na Mauaji mbalimbali katika eneo la Meru ambapo watu 3 wameshafikishwa mahakamani huku wengine wakiwa wanaendelea na uchunguzi  katika  tukio la kuuwa vibaya kwa Kada wa Chadema wiki chache zilizopita.
Pia alisema kuwa mbali na kuweza kuwashikilia watu 12 ambao wanahusika na  mauaji ya Kada wa Chadema pia bado jeshi hilo linaendelea na upelelezoi zaidi ili kuweza kuwatia mbaroni pia waliohusika na mauaji ya bibi kizee Bi Martha Joseph(77) kwa madai kuwa alikuwa ni mchawi katika eneo la Nkoaranga
kwa hisani ya fullshangwe

No comments:

Post a Comment