Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, May 27, 2012

Dr Mwakyembe Akesha Stesheni Ya Tazara na abiria



WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe  juzi usiku alikesha na abiria zaidi ya 1,000 waliokwama kwa saa 11 katika stesheni ya Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (Tazara) jijini Dar es Salaam kutokana treni kukosa mafuta.
 
Kutokana na tatizo hilo, Dk Mwakyembe ambaye alifika katika stesheni hiyo mara baada ya kuwasili kutoka safarini India, aliahidi kuwashughulikia watendaji wa Tazara waliosababisha uzembe huo.
Dk Mwakyembe ambaye ametimiza siku 20 tangu alipoteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuongoza Wizara ya Uchukuzi, alifika eneo hilo baada ya abiria wawili kumpigia simu na kuomba aingilie kati tatizo hilo.
 Alifika stesheni katika hiyo saa 4:01 usiku na kukaa mpaka saa 6:30 usiku alipoondoka na hakukuwa na  kiongozi yeyote wa ngazi za juu wa Tazara aliyefika kushughulikia tatizo hilo.   

 Akutana na abiria Baada ya Dk Mwakyembe kuwasili na kuingia katika ukumbi wa kupumuzika abiria wanaposubiri kuondoa, wasafiri walimshangilia kwa nguvu mara baada ya kujitambulisha kuwa ni Waziri wa Uchukuzi na amefika kutatua tatizo linalowakabili, ingawa ni usiku akiwa ametoka safarini India.
Abiria hao waliokuwa na  jazba walimwelezea waziri huyo kuwa kufika kwake eneo hilo ni uzalendo ambao hawakuutegemea na kutaka awapatie majibu ya chanzo cha tatizo na namna atakavyolitatua.
 
Awali, Kabla ya kuingia ndani ya ukumbi huo, uliibuka mvutano wa chini kwa chini baina yake na baadhi ya watendaji na  wanausalama waliotaka asingie ukumbini  kwa hofu ya kufanyiwa vurugu abiria hao waliokuwa na hasiri.
Lakini Dk Mwakyembe aliwataka watendaji wamfungulie mlango ili aingie ndani ya ukumbi kukutana na abiria hao.
 
Alipofunguliwa mlango, Dk Mwakyemba akiwa ameongozana na baadhi ya wafanyakazi wa mamlaka hiyo waliokuwa zamu, aliingia ndani ya ukumbi na umati wa watu  walimzunguka huku kila mmoja akitaka kuwakilisha kilio chake.

Mmoja wa abiria hao alipasa sauti na akisema; “Tunataka uje huku, mpaka muda huu hatujaondoka,  hatuelewi chochote, hatujui kama treni itaondoka au hapana, na kama itaondoka itakuwa saa ngapi? Hawa Tazara wanadharau, wanatutesa! Tunaomba uje utusikilize na ueleze kama safari ipo au la”.   Dk Mwakyembe aliwatuliza akisema; “Tulieni, tulieni! Nimekuja hapa kwa sababu baadhi yenu wamenipigia simu kunieleza kuwa mmekwama hapa kwa muda mrefu na mnahiji  msaada ili muweze kuondoka.
 
“Mimi ndiye Waziri wa Uchukuzi, nimekuja kujionea mwenyewe na kuchukue  hatua. Ninawaahidi hali hii  katika kipindi hiki cha uongozi wangu haitajirudia.
Nitahakikisha ndani ya muda mfupi kunakuwa na mabadiliko makubwa.”
 
Baada ya maelezo hayo, abiria hao walianza kuzungumza  kwa mpangilio na kumweleza waziri huyo kuwa kitendo cha treini ya abiria kuchelewa kuondoka bila taarifa yoyote kinawasababisha usumbufu mkubwa.
Mmoja wa abiria hao, Paulo Michael alisema kama hali hiyo haitadhibitiwa inaweza kulipeleka taifa katika hali mbaya kwa kuwa wananchi wamechoka  na kukataa tamaa.
 
“Mheshimiwa hivi sasa wananchi wamekata tamaa, kama watendaji wa mamlaka hii  wataendelea kututesa namna hii …alilalamika Michael ambaye alionekana kukerwa na kitendo hicho.
Alisema watu wakiwamo wanawake na watoto, wanateseka kutokana na  uzembe wa watu wachache na kwamba, jambo hilo ni hatari kwa usalama wa nchi.
 
Akijibu hilo, Dk Mwakyembe alisema; “Kuhusu hili nawahakikishia kuwa halitatokea tena katika kipindi changu, natambua mmeumia, lakini nawaahidi kufanya mabadiliko, nipeni muda mfupi.” 
Abiria hao waliendelea kupaza sauti wakimtaka waziri huyo kutoondoka eneo hilo hadi watakapoondoka kwa kuwa watendaji hao wanaweza kuwadanganya.

Hata hivyo, Waziri Mwakyembe kabla ya ombi hilo la abiria alikuwa ameahidi kuwa hataondoka eneo hilo hadi treni litakapoondoka.
 Dk Mwakyembe

No comments:

Post a Comment