Hizi
ni baadhi ya vurugu zilizotokea jana Mjini Zanzibar huku mabomu ya
machozi yakirindima na kuendelea kupigwa na polisi wakati wa vurugu
zilizoshababishwa na kundi kubwa la watu kwenda kuvamia kituo cha polisi
ili kushinikiza kiongozi wao aliyeshikiliwa na jeshi la polisi aachiwe
huru
Picha
askari wa kutuliza ghasia akiwa tayari kwa mapambano n awananchi wa
zanzibar ambao inasemekana walivamia kituo cha polisi wakiwa na silaha
za jadi kama vile rungu na mapanga
Hali
tete bado inaendelea asubuhi ya leo mjini zanzibar huku polisi
wakiwatawanya wananchi wa zanzibar lakini wananchi hao wanazidi
kuongezeka kwa kutaka kiongozi wao kuachiwa huru na polisi ambapo
alikamatwa jana na wananchi hao kuvamia kituo cha polisi jana jioni na
hatimaye polisi kutumia mabomu ya machozi tokeaa jana jioni hadi asubuhi
ya leo
Wananchi
wa Zanzibar wakiwa kwenye maandamano wakati wakielekea kituo cha polisi
na kabla machozi ya mabomu hayajaanza kulipuliwa na askari.Picha Zote
na Abdulaziz El ShuwehdyJANA JIONI KUNDI KUBWA LA WATU WANAOLIUNGANISHA KUNDI LIFAHAMIKALO KWA JINA LA UAMSHO,AMBALO LIMEKUWA LIKIUPIGA VITA MUUNGANO WA TANZANIA NA ZANZIBAR,LILIVAMIA KITUO KIKUU CHA POLISI CHA MADEMA KISIWANI HUMO JIONI YA JANA NA KUSABABISHA VURUGU KUBWA,WAKITAKA KUACHILIWA KWA KIONGOZI WAO ALIEKAMATWA JIONI YA JANA KWA KUONGOZA MHADHARA BILA YA KUWA NA KIBALI CHA SERIKALI.
HALI HIYO IMESABABISHA VURUGU KUBWA KITUONI HAPO HUKU ASKARI POLISI WA KITUO HICHO WAKILAZIMIKA KUTUMIA MABOMU YA MACHOZI ILI KUWATAWANYA WATU HAO AMBAO WENGI WAO WAKO NA SILAHA ZA JADI AMBAZO NI MARUNGU,MAPANGA NA MAWE ILI KUPAMBANA NA ASKARI POLISI KITUONI HAPO VURUGU HIZO ZIMEENDELEA TENA ASUBUHI YA LEO.source lukaza
No comments:
Post a Comment