Siku
mbili baada ya magazeti na baadhi ya vyombo vya habari kueneza story
kwamba kiungo wa zamani wa Mtibwa Sugar ambaye alikuwa nje akicheza
Vancouver Whitecaps kabla ya kuhamia Philadephia - Nizar Khalfan kwamba
amesaini miaka 2 kuichezea Yanga, leo nimeongea na Nizar mwenyewe ambaye
amekana kutia saini ya aina yoyote na klabu ya jangwani.
"Kiukweli
nimesikitishwa sana na hizi taarifa kwamba sijui nimesaini kuichezea
Yanga kwa sababu ni mambo ambayo hayana ukweli kabisa. Mwanzoni
ilisemekana nimesaini Simba lakini haikuwa ukweli, sikatai nimeshafuatwa
na baadhi ya timu hapa Tanzania nijiunge nazo lakini na mimi naangalia
vigezo vyangu ndipo nitakapochukua maamuzi. Lengo langu ni bado niende
nikacheze nje ya nchi katika soka la kulipwa, hivyo hata kama ikitokea
nimejiunga na timu yoyote ni lazima mkataba uwe wa muda mfupi ambao
utakuwa na vipengele ambavyo havitakuwa na vikwazo vinavyoweza kunifanya
nisitimize malengo yangu ya kwenda kucheza nje. Hali halisi kwa sasa
ipo hivyo, sina timu kwa sasa hata mazoezi nafanya pale muhimbili na
timu ya Binslum." - alisema Nizar Khalfan.
kwa hisani ya shaffih dauda blog
kwa hisani ya shaffih dauda blog
No comments:
Post a Comment