Siku
moja baada ya kutua Tanzania akitokea Sudan na klabu yake ya Simba
katika michuano ya kombe la shirikisho na kuzuka kwa habari kwamba
amejiunga na klabu Yanga, Kelvin Yondani ameongea exclusively na www.shaffihdauda.com na kukanusha taarifa kwamba anahamia mitaa ya jangwani kutoka Msimbazi.
Kelvin
ambaye mwaka jana pia alikuwa akihusishwa na taarifa za kujiunga na
Yanga amesema yeye bado ni mchezaji halali wa mabingwa wa Tanzania na
ataendelea kuwepo Msimbazi kwa misimu miwili zaidi, "Jana
nilivyorudi kutoka Sudan nimekuwa nikipokea simu nyingi za waandishi
wakiulizia ukweli juu ya taarifa za kujiunga na Yanga lakini sikuwa
nimepata wakati mzuri wa kuwajibu. Leo kupitia www.shaffihdauda.com
natangaza rasmi kwamba mie ni mchezaji wa na nitakuwa hivyo kwa misimu
miwili ijayo kwa sababu nimeongeza mkataba wa kuitumikia klabu yangu kwa
miaka zaidi. Hivyo hizo taarifa si za kweli mie bado nipo kwenye
winning team."
kwa hisani ya shaffih dauda blog
No comments:
Post a Comment