Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, May 28, 2012

Fredrick Sumaye asena : Rushwa imekithiri nchini



Na Dotto Mwaibale

WAZIRI Mkuu mstaafu wa Awamu ya Tatu, Frederick Sumaye amesema vitendo vya rushwa vimekithiri nchini na kubainisha kuwa nchi haiwezi kusonga mbele kwa kukumbatia vitendo hivyo.
 
Sumaye aliyasema hayo kwenye ibada ya kuliombea Taifa iliyofanyika Kanisa la Ufufuo na Uzima la Kawe Tanganyika Peackars Dar es Salaam leo.
Alisema jambo la pekee la kuleta amani nchini ni wananchi wenyewe kubadilika na kuacha vitendo vya kukumbatia rushwa na  ufisadi.
"Vitendo vya rushwa vimekithiri sana katika nchi yetu hasa katika chaguzi mbalimbali mkipewa chukueni lakini msiwape kura," alisema Sumaye.
Alisema maombi yanayofanywa na viongozi wa dini mbalimbali  yanawasaidia waumini wao kujua ni kitu gani kitakachosaidia kuacha kupokea rushwa.
Sumaye alisema viongozi wanaochaguliwa kwa kutoa rushwa wanapaswa kuogopwa kwani malengo yao ni kujinufaisha wao na si kuwatumikia wananchi.
Aliwataka wananchi kuwa majasiri wa kupiga vita vitendo hivyo kwa vitendo ingawa alisema wataonekana ni wabaya machoni pa jamii.
"Vita vya rushwa si vya kuwaachia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) peke yao bali kila mtu mahali alipo apambane," alisema Sumaye.
Mchungaji Msaidizi wa Kanisa hilo, Gwandu Mwangasa alisema nchi ina rasilimali nyingi lakini zinawanufaisha wachache kutokana na kukithiri kwa vitendo vya rushwa na kifisadi ambapo aliwataka waumini mbalimbali kuwakataa viongozi wanaoabudu rushwa.

No comments:

Post a Comment