MALKIA wa Disco, Donna Summer amefariki dunia leo akiwa ana umri wa miaka 63 baada ya kusumbuliwa na maradhi ya saratani kwa mwaka mzima.
Mshindi huyo wa tuzo tano za Grammy alikuwa mjini Florida wakati anafariki dunia.
Donna alijipatia
umaarufu enzi 'majoka' miaka ya 1970 na alikuwa maarufu kutokana na
vibao vilivyotikisa kama Love To Love You, I Feel Love na Hot Stuff -
ambao ulitumika katika filamu ya The Full Monty.
Ameacha mume, mwimbaji
na mtayarishaji Bruce Sudano, watoto wao wa kike Brooklyn na Amanda na
mwingine wa Summer, Mimi, aliyempata katika mahusiano mengine.
Alizaliwa kwa jina la Donna Adrian Gaines mjini Boston, Massachusetts na muziki alianzia kanisani kwenye kwaya.
Mwalimu mama yake
alisema alianza kuimba mara tu alipoanza kuzungumza. Mwishoni mwa miaka
ya 1960, Donna alianzisha vikundi kadhaa vkabla ya kwenda Ujerumani kwa
shughuli za kimuziki pia.
Kisha akasaini mkataba wa kurekodi na kutoa albamu yake ya kwanza, Lady of the Night mwaka 1974
No comments:
Post a Comment