Rafiki wa karibu na marehemu ambaye amenusurika kwenye ajali hiyo (kulia) akilia kwa uchungu.
Mchezaji wa Simba, Haruna Moshi ‘Boban’ (kulia), akiwa wamekaa kwa huzuni na wenzake.
Boban akilia kwa uchungu.
Waombolezaji ambao ni mashabiki zake wakilia kwa uchungu.
Kifo cha kiungo mkabaji wa timu ya Simba, Patrick Mafisango,
kilichotokea leo alfajiri maeneo ya Veta-Chang’ombe jijini Dar es
Salaam baada ya kupata ajali ya gari, kimewahuzunisha watu wengi
ambao walikusanyika nyumbani kwa mchezaji mwenzake, Emannuel Okwi,
maeneo ya Bora-Keko ambako taratibu za msiba zinafanyika huku wakilia
kama watoto.
Ndugu yake Mafisango aliekua nae wakati wa ajali
amesema Mafisango alifariki dunia hapohapo kwenye ajali wakati wakitoka
Club kuelekea nyumbani, walipofika kwenye taa za barabarani Tazara Dar
es salaam, Mafisango ambae ndio alikua anaendesha alijaribu kuziwahi taa
lakini ghafla akakutana na mwendesha guta ambapo katika kumkwepa gari
ilimshinda na kuingia mtaroni leo Alfajiri.
Alikua na wenzake watano
kwenye gari ambapo wengine wanne wamepona japoa walipata majeraha madogo
madogo akiwemo mdogo wake ambae amesajiliwa na club ya Simba.
Haruna Niyonzima mchezaji
wa Yanga alikua mchezaji wa mwisho kubadilishana jezi na Mafisango
Tanzania, katika mechi ambayo Mafisango alifunga goli lake la mwisho.
Anasema Ijumaa ndio
Mafisango alimwambia atasafiri kwenda Rwanda kujiunga na kikosi cha timu
ya taifa, hili ni pigo kwa Tanzania, Rwanda na hata Congo DRC.
picha na matukio kwa hisani ya global publisher
No comments:
Post a Comment