YUSUFF
Mehboob Manji (pichani kushoto), ameibuka tena Yanga, baada ya kimya
cha muda mrefu akijitokeza kwa nia ya kuokoa jahazi kutokana hali mbaya
ya kiuchumi inayoikabili klabu kwa sasa.
Waajiriwa
wa Yanga, wakiwemo makocha, wachezaji na watendaji hawajalipwa
mishahara kwa takriban miezi minne, hali inayoashiria uongozi wa klabu
hiyo, chini ya Mwenyekiti wake, Wakili Lloyd Baharagu Nchunga
umeelemewa.
Lakini mfanyabiashara kijana anayemiliki mamilioni ya fedha, Manji yu tayari kuokoa jahazi kwa kurejesha udhamini katika klabu.
Hata hivyo, ili kurejea kuidhamini Yanga, Manji ametoa masharti matano.
Masharti
hayo ni; kufanyika uhakiki wa mahesabu ya akaunti za Yanga ndani ya
siku 90 na wakaguzi wa hesabu wa kujitegemea kukagua hesabu za kipindi
cha kuanzia mwaka 2006 hadi 2012 kwa ajili ya fedha zilizoingia klabuni.
Sharti la pili ni kuchapishwa magazetini kwa akaunti za Yanga siku 15 baada ya kumalizika kwa robo ya mwaka, tatu ni
kuendeshwa
zoezi la kura ya maoni ndani ya siku 60 na kuamua kama wanachama wa
Yanga wanataka klabu iwe Yanga au la na sharti la nne ni mabadiliko ya
Katiba ndani ya siku 90.
Kwa mujibu wa barua ya Manji kwa Mwenyekiti wa Yanga, Nchunga ambayo blogu hii imeipata
nakala yake, ameutaka pia uongozi kuidhinisha mgombea wa nafasi ya
Mwenyekiti wa klabu, nafasi ambayo iko wazi baada ya Davis Mosha
kujiuzulu mwaka jana.
Sharti la mwisho la Manji ni kutaka kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa wanachama ndani ya siku 30, ili kujadili mustakabali wa klabu.
No comments:
Post a Comment