Mabingwa watetezi Hispania |
MICHUANO
ya Kombe la Mataifa ya Ulaya, Euro 2012 inayoandaliwa kwa pamoja na
Poland na Ukraine itakuwa ni fainali za 14 za michuano hiyo kufanyika.
Lilikuwa
ni wazo la Henri Delaunay, Katibu wa Shirikisho la Soka Ufaransa,
ambaye aliibuka na wazo hilo kwa mara ya kwanza kwenye bara hilo, mwaka
1927.
Kwa
mara ya kwanza alipata sapoti kidogo sana na michuano hiyo haikuanza
hadi mwaka 1960. Hadi mwaka 1980 ni timu nne tu zilikuwa zinacheza hatua
ya fainali, lakini sasa ni timu 16 na imekuwa moja ya michuano mikubwa
katika kalenda ya soka.
Michuano yote 13 iliyotangulia imeacha kumbukumbu kibao – dj-sek inakuletea wasifu wa michuano hiyo hadi kufikia fainali za mwaka huu.
Mfungaji wa bao la ubingwa fainali zilizopita za Euro,Torres amerejeshwa kikosini dakika za mwishoni, je atang'ara tena? |
1960
MICHUANO
ya kwanza ilifanyika Ufaransa na bingwa alikuwa Soviet Union. Mabingwa
hao waliongozwa na kipa wao gwiji, Lev Yashin langoni kwenye michuano
hiyo. Kipa aliyeipa England taji la Kombe la Dunia, Gordan Banks
alifunikwa na kipa huyo.
1964
Hispania
kwa sasa wanatawala katika ulimwengu wa soka, lakini mafanikio yao ya
kwanza yalikuja katika Euro ya 1964, wakati walipotwaa taji hilo kwenye
ardhi ya nyumbani katika timu iliyoongozwa na Luis Suarez. Kiungo huyo
aling’ara kwenye michuano hiyo, ambayo Hispania ilifunika mbaya.
1968
Michuano
ya tatu ya Ulaya ilifanyika Italia na kama ilivyokuwa Hispania 1964,
pia michuano hii ubingwa ulichukuliwa na wenyeji. England ilifika Nusu
Fainali na ilifungwa na Yugoslavia katika mechi ya kusisimua, iliyokuwa
na upinzani mkali. Alan Mullery wa England alionyeshwa kadi nyekundu
kwenye mechi hiyo.
1972
Waliokuwa
mabingwa watetezi wa Ulaya, Italia walishindwa kufuzu kuingia kwenye
fainali hizo, wakiangushwa na Ubelgiji waliokuwa wenyeji, katika Robo
Fainali. Pamoja na hayo, Ujerumani waliweza, waliwafunga wenyeji hao na
kufuzu kutinga fainali za michuano hiyo, ambako waliifunga iliyokuwa
USSR mabao 3-0 na kutwaa Kombe.
1976
Michuano
‘iliyong’ara’ ya Euro 1976 taji lilichukuliwa na Czechoslovakia
walioifunga Ujerumani Magharibi kwenye fainali kwa mikwaju ya penalti
mjini Belgrade. Lakini pia ilikuwa michuano ambayo Wales ilikaribia
kufuzu.
1980
Mfumo
wa michuano ulibadilika mwaka 1980, kwa timu nane kuingia kwenye
fainali, lakini mwonekano wa matokeo haukubadilika, kwa Ujerumani kutwaa
ubingwa. Pamoja na hayo, kulikuwa kuna ‘maajabu’ kadhaa ikiwemo
Ubelgiji iliyokuwa na vipaji babu kubwa kufika fainali, mmojawao akiwa
ni Jean-Marie Pfaff.
1984
Ufaransa
walikaribia kutwaa taji la Kombe la Dunia mwaka 1982, kabla ya
kupokonywa tonge mdomoni na Ujerumani Magharibi katika Nusu Fainali ya
kukumbukwa, lakini hakukuwa na maajabu katika ardhi ya nyumbani, wakati
Wafaransa walipoongozwa na gwiji wake Michel Platini kutwaa taji hilo.
1988
Ilikuwa
ni michuano ambayo mshambuliaji wa Uholanzi, Marco van Basten alikuwa
hana wa kumfananisha naye, kutokana na kufunga mabao ambayo yaliiwezesha
nchi yake kutwaa Kombe. Pamoja na hayo, ilikuwa habari tofauti kwa
USSR, iliyoongozwa na kocha wake gwiji, Valery Lobanovsky walipokaribia
kutwaa taji.
1992
Denmark
haikufuzu kwenye fainali hizo nchini Sweden, lakini walipata nafasi
kutokana na Yugoslavia kuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe, hivyo
kushindwa kushiriki. Na vijana hao wakafanikiwa kutwaa ubingwa wa
michuano hiyo, wakiifunga Ujerumani kwenye fainali. Kim Vilfort, ambaye
alifunga kwenye fainali alielezea namna ambavyo Denmark walikuwa na
maandalizi mazuri kabla ya fainali hizo.
1996
Euro
96 – michuano ambayo ilipewa jina soka imerejea nyumbani. England
ilifika Nusu Fainali, lakini ikafungwa na Ujerumani kwa mikwaju ya
penalti. Ujerumani ilifanikiwa kutwaa taji hilo kwa kuifunga Czechs
Uwanja wa Wembley. Mshambuliaji wa England, Alan Shearer alifanya vitu
adimu sana kwenye fainali hizo.
2000
England
ilifanikiwa kuifunga Ujerumani, lakini hawakufanikiwa kufuzu kutoka
kwenye kundi lao na vijana wa Kevin Keegan walirejeshwa nyumbani
kimaajabu. Ufaransa walitwaa Kombe la Dunia nyumbani kwao mwaka 1998 na
wakadhihirisha ubabe wao kwa kutwaa taji la Ulaya pia kwenye fainali
zilizoandaliwa kwa pamoja na Ubelgiji na Uholanzi. Kiungo Emmanuel Petit
aliyeng’ara kwenye michuano hizo alielezea siri ya mafanikio ya nchi
yao.
2004
Euro
2004: Ugiriki walipoibuka mabingwa. Ilikuwa unakwenda kuwa mwaka wa
Ureno, katika fainali ambazo walikuwa wenyeji, lakini wakafungwa na
Ugiriki 1-0 kwenye fainali. Cristiano Ronaldo aliumizwa sana na matokeo
hayo, kwani ulikuwa mwaka wa kufurahia mafanikio na timu yake ya taifa,
lakini ikashindikana.
2008
Katika
michuano iliyoandaliwa kwa pamoja na Uswisi na Austria, ambayo ilifana,
Hispania waliibuka mabingwa baada ya miaka 44 ya kusubiri taji la
kimataifa. Hispania waliifunga 1-0 Ujerumani katika fainali, bao pekee
la Fernando Torres dakika ya 33 na sasa wanaingia kwenye fainali za
mwaka huu kutetea taji, wakiwa pia mabingwa wa dunia. Je, wataweza? Bila
shaka hilo ni jambo la kusubiri na kuona.
No comments:
Post a Comment