Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, May 13, 2012

JENGO LA MKUU WA WILAYA ARUSHA LAKOSA CHOO, KILICHOPO KIMEJAA NA MAJI MACHAFU YANATAPAKAA HOVYO KUZUNGUKA JENGO HILO


Na Gladness Mushi wa Fullshangwe-Arusha
WAFANYAKAZI katika jengo la mkuu wa wilaya ya Arusha wamelalamikia ukosefu wa choo kwa muda mrefu wakidai afya zao zipo hatarini kukumbwa na mlipuko wa magonjwa,kufuatia  choo kilichopo kuziba na kusababisha mazingira ya ofisi hiyo kutapakaa maji machafu yenye  harufu kali na vinyesi .

Suala hilo limekuwa likilalamikiwa kwa zaidi ya mwaka mmoja bila kupatiwa ufumbuzi huku wafanyakazi hao wakiendelea kukumbwa na adha ya  harufu kali sanjari na kukanyaga maji machafu kila siku wakati wakiingia ofisini kwao.

Wakizungumza na waandishi wa habari kwa sharti la kutonukuliwa majina yao na vyombo vya habari,walisema kuwa adha hiyo imekuwa ikiwakumba zaidi watumishi waliopo chini ya jengo hilo ,ambapo watumishi walipo juu gorofani wamekuwa wakimwaga  maji na kusababisha choo cha chini  kutapisha maji machafu vyenye vinyesi na kuzagaa eneo  la jingo hilo.

‘’kama mnavyoona hii hali inatisha kwani muda mrefu sana hiki choo kimeziba wenzetu wakimwaga maji huko juu ,uchafu wote unatoka nje  na kutapakaa kila kona vikiwemo vinyesi ,mipira ya kiume (condom),na pedi za akina mama vinazagaa ovyo’’alisema mmoja wa watumishi katika jingo hilo idara ya elimu

Wafanyakazi hao kutoka idara m,balimbali za serikali katika jingo hilo wamedai kuwa wamekuwa wakipata shida mahala pa kujisaidia na kulazimika kwenda umbali mrefu kutafuta huduma hiyo ya choo.

Aidha wamedai taarifa juu ya ubovu wa choo hicho walishaitoka kwa viongozi kadhaa wa wilaya waliopo katika jengo hilo akiwemo mkuu wa wilaya Raymond Mushi na katibu tawala wa wilaya Emi Lyimo,bila kupatiwa ufumbuzi .

Kukosekana kwa huduma ya choo katika jengo hilo kumewakumba watumishi wa idara mbalimbali za serikali  ambao ni  pamoja na Baraza la Ardhi wilaya,Ofisi ya mshauri wa migambo,Hazina ndogo ,Elimu mkoa,Mkaguzi wa elimu kanda ya mashariki,ofisi ya wazee na ofisi ya mbunge.

Akizungumzia hali hiyo katibu tawala wa wilaya Emi Lyimo alikiri kupata taarifa juu ya uboivu wa choo hicho ,lakini alidai kuwa suala hilo lipo juu yak e na tayari taarifa walishazifikisha kunakohusika ofisi ya katibu tawala mkoa ambaye ndie mwenye mwenye dhamana ya jengo hilo.

Alisema kuwa hali ya ubovu wa choo hicho ni ya siku nyingi hata mkuu wa wilaya amekuwa akikumbwa na adha kutokana na harufu kali inayoingia ofisini kwake na kujikuta akishindwa kufanyakazi kwa ufanisi,hali ambayo ilimlazimu kuitisha vikao mara kadhaa kuzungumzia hali hiyo.

Kwa upande wa katibu tawala mkoa wa Arusha,Everin Itanisa ,baada ya kuhojiwa juu ya ubovu wa choo katika jengo hilo alidai kuwa taarifa hizo anazo ,kilichokuwa kikikwanisha kufanyika kwa marekebisho ni ukosefu wa fedha .

Alisema kuwa mradi wa ukarabati wa choo hicho unagharimu kiasi cha shilingi milioni 12 na ofisi yake haikuwa na fedha ila wamepata nusu yake baada ya kuamua kuachangisha katika idara zote katika ofisi ya mkuu wa mkoa, kutokana na serikali kutokuwa na fedha.

No comments:

Post a Comment