Na Gladness Mushi wa Fullshangwe-Arusha
WAFANYAKAZI katika jengo la mkuu wa wilaya ya Arusha
wamelalamikia ukosefu wa choo kwa muda mrefu wakidai afya zao zipo hatarini
kukumbwa na mlipuko wa magonjwa,kufuatia choo kilichopo kuziba na kusababisha mazingira
ya ofisi hiyo kutapakaa maji machafu yenye harufu kali na vinyesi .
Suala hilo limekuwa likilalamikiwa kwa zaidi ya mwaka
mmoja bila kupatiwa ufumbuzi huku wafanyakazi hao wakiendelea kukumbwa na adha
ya harufu kali sanjari na kukanyaga maji
machafu kila siku wakati wakiingia ofisini kwao.
Wakizungumza na waandishi wa habari kwa sharti la
kutonukuliwa majina yao na vyombo vya habari,walisema kuwa adha hiyo imekuwa
ikiwakumba zaidi watumishi waliopo chini ya jengo hilo ,ambapo watumishi walipo
juu gorofani wamekuwa wakimwaga maji na
kusababisha choo cha chini kutapisha
maji machafu vyenye vinyesi na kuzagaa eneo
la jingo hilo.
‘’kama mnavyoona hii hali inatisha kwani muda mrefu sana
hiki choo kimeziba wenzetu wakimwaga maji huko juu ,uchafu wote unatoka
nje na kutapakaa kila kona vikiwemo
vinyesi ,mipira ya kiume (condom),na pedi za akina mama vinazagaa ovyo’’alisema
mmoja wa watumishi katika jingo hilo idara ya elimu
Wafanyakazi hao kutoka idara m,balimbali za serikali
katika jingo hilo wamedai kuwa wamekuwa wakipata shida mahala pa kujisaidia na
kulazimika kwenda umbali mrefu kutafuta huduma hiyo ya choo.
Aidha wamedai taarifa juu ya ubovu wa choo hicho walishaitoka
kwa viongozi kadhaa wa wilaya waliopo katika jengo hilo akiwemo mkuu wa wilaya
Raymond Mushi na katibu tawala wa wilaya Emi Lyimo,bila kupatiwa ufumbuzi .
Kukosekana
kwa huduma ya choo katika jengo hilo kumewakumba watumishi wa idara
mbalimbali za serikali ambao ni pamoja na Baraza la Ardhi wilaya,Ofisi
ya mshauri wa migambo,Hazina ndogo ,Elimu mkoa,Mkaguzi wa elimu kanda
ya mashariki,ofisi ya wazee na ofisi ya mbunge.
Akizungumzia hali hiyo katibu tawala wa wilaya Emi Lyimo
alikiri kupata taarifa juu ya uboivu wa choo hicho ,lakini alidai kuwa suala
hilo lipo juu yak e na tayari taarifa walishazifikisha kunakohusika ofisi ya
katibu tawala mkoa ambaye ndie mwenye mwenye dhamana ya jengo hilo.
Alisema kuwa hali ya ubovu wa choo hicho ni ya siku
nyingi hata mkuu wa wilaya amekuwa akikumbwa na adha kutokana na harufu kali
inayoingia ofisini kwake na kujikuta akishindwa kufanyakazi kwa ufanisi,hali
ambayo ilimlazimu kuitisha vikao mara kadhaa kuzungumzia hali hiyo.
Kwa upande wa katibu tawala mkoa wa Arusha,Everin
Itanisa ,baada ya kuhojiwa juu ya ubovu wa choo katika jengo hilo alidai kuwa
taarifa hizo anazo ,kilichokuwa kikikwanisha kufanyika kwa marekebisho ni
ukosefu wa fedha .
Alisema kuwa mradi wa ukarabati wa choo hicho unagharimu
kiasi cha shilingi milioni 12 na ofisi yake haikuwa na fedha ila wamepata nusu
yake baada ya kuamua kuachangisha katika idara zote katika ofisi ya mkuu wa
mkoa, kutokana na serikali kutokuwa na fedha.
No comments:
Post a Comment