Mahakama
ya Hakimu mkazi Kisutu imelikataa ombi la Mawakili wanaomtetea
mtuhumiwa wa mauaji ya muigizaji wa filamu nchini Marehemu STEVEN
KANUMBA, ELIZABETH MICHAEL maarufu kwa jina la LULU la kutaka kesi hiyo
isikilizwe katika mahakama ya watoto kutokana na mtuhumiwa huyo kuwa na
umri wa chini ya miaka 18.
Akizungumza mahakamani hapo Hakimu mfawidhi AUGUSTINE
MMBANDO wa Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu, amesema ELIZABETH
anakabiliwa na kosa la mauaji na mahakama hiyo haina mamlaka ya
kusikiliza kesi za mauaji isipokuwa mahakama Kuu na kuwataka kupeleka
ombi hilo katika mahakama hiyo.
Awali
wakili wa Serikali katika kesi hiyo ELIZABETH KAGANDA baada ya kupokea
cheti cha kuzaliwa cha ELIZABETH amesema ipo haja yak kufanyika kwa
uchunguzi kuhusiana na umri wa mshitakiwa huyo kutokana na maelezo
aliyoandika polisi wakati alipokamatwa kuwa ana umri wa miaka 18 wakati
cheti hicho kinaonyesha ana umri wa miaka 17.
Wakili
huyo pia amesema katika cheti hicho limeandikwa jina la DIANA ELIZABETH
wakati mtuhumiwa alitaja jina lake kuwa ni ELIZABETH MICHAEL jambo
ambalo mawakili wa upande wa utetezi, wamesema mara nyingi wakristo huwa
wanatumia majina mawili na kudai kuwa cheti hicho ni halali.
Kesi hiyo itatajwa tena Mei 21, mwaka huu ambapo uchunguzi bado haujakamilika.
No comments:
Post a Comment