NA MWANDISHI WETU
MKURUGENZI Mtendaji wa Hospitali ya Saratani Ocean
Road, Twalibu Ngoma amekiri kuwa kuanguka kwa huduma za matibabu katika
hospitali hiyo, kumechangiwa na uwezo mdogo wa serikali wa kununua
mashine za mionzi kwa ajili ya
wagonjwa hao.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es
Salaam leo Mkurugenzi huyo aliwataka watanzania kufahamu kuwa hadi sasa
hospitali hiyo ina mashine moja ambayo haiendani na idadi ya wagonjwa wanaofika
hospitalini hapo.
Ngoma alisema ili huduma hizo ziweze kuwa za
uhakika, hospitali hiyo inapaswa kuwa na mashine nane (8), ambapo kwa sasa ipo
mashine moja ambayo haikidhi.
“Unajua gharama za kununua mshine moja hadi kufungwa
inafikia gharama ya shil. Bilioni 2, fedha ambazo kwa sasa serikali haina uwezo
wa kuzipata mara moja”alisema Ngoma.
Ngoma alisema kutokana na uwepo wa mashine hiyo moja
kumesababisha wagonjwa zaidi ya 100 hadi 200 kulazimika kupatiwa huduma hiyo ya
mionzi kitendo ambacho hakilingani na matibabu hayo.
Alisema takwimu zinaonyesha kuwa kila mwaka kuna
wagonjwa 40000 wanaohitaji kupatiwa matibabu lakini hata hivyo kati ya hao ni
4000 pekee ndio wanaopati huduma hiyo.
Aliwataka Wanzania kutambua kuwa kuanguka kwa huduma
za matibabu ya saratani katika katika hospitali hiyo hakutokani na mtu bali
kunasababishwa na uwezo mdogo wa kifedha wa serikali.
Akizungumzia matatizo ya manesi ya kutishia
kuandamana kutokana na kutolipwa malipo ya saa za ziada za kazi, Mkurugenzi
huyo alisema hiyo ni moja ya haki yao ya msingi ili mradi wawe na sababu za
msingi.
Alisema kima inavyoeleweka kuwa hospitali hiyo haina
kibali cha kulipa malipo ya ziada ambapo hadi sasa hakuna Nesi anayefanya baada
ya masaa ya kawaida (overtime).
kwa hisani ya fullshangwe
No comments:
Post a Comment