Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, May 24, 2012

MBUNGE WA ROMBO,MH JOSEPH SELASINI APATA AJALI MBAYA JIONI YA LEO



Mbunge wa Rombo, Mhe. Joseph Selasini amepata ajali mbaya  sana wakati alipokuwa akiendesha gari lake mkoani Kilimanjaro, ambapo watu 3 kati ya watu 6 waliokuwemo kwenye gari hilo hali zao ni mbaya na wamechukuliwa na gari la polisi kupelekwa hospitali.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Kamada Absalom Mwakyoma amesema kwa sasa hawezi kuthibitisha kwamba ni watu wangapi wamepoteza maisha katika ajali hiyo kwani daktari ndiyo mwenye dhamana ya kuthibitisha kifo.



Amewataka waandishi wa habari wawe watulivu wasubiri kidogo kwa sasa, taarifa zaidi atazitoa muda mfupi ujao baada ya kujua hali halisi ya tukio hilo kwani kwa sasa yuko njiani akielekea eneo la tukio.

No comments:

Post a Comment