Pages

Friday, May 25, 2012

MZEE SMALL ALAZWA HOSPITALI

Anafahamika kama Said Ngamba maarufu kwa jina la Mzee Small ambaye hivi sasa amelazwa kwenye hospitali ya Amana kwa matibabu ya afya yake baada ya kupata ugonjwa wa ghafla aliporejea Dar kutoka kwenye ziara yake mkoani Mwanza Mei 21 mwaka huu. Mzee Small ambaye alikuwa na Bi. Chau mkoani Mwanza alipatwa na ugonjwa ambao haukuweza kufahamika haraka baada ya kurejea nyumbani kwake Tabata ambapo baada ya kufika alionekana kama amechanganyikiwa huku akiwa hawezi kuongea na mkono wake mmoja ukiwa unashindwa kufanya kazi kama kawaida yake, Lakini alipofikishwa hospitali Daktari alisema
amepatwa na stroke ambayo ni dalili za ugonjwa wa kiharusi. Habari na Globalpublishers.

No comments:

Post a Comment