wachungaji wa kanisa la FPCT wakiwa wanawaombea wabange walioudhuria
katika sherehe hizo za shukurani akiwemo mbunge mwenyeji Joshua Nassari
mbunge wa arumeru mashariki,mbunge wa iringa mjini mchungaji peter
msingwa pamoja na mbunge Kingi Lugola kutoka Mara ambapo wote walikula
kiapo cha kukataa rushwa
picha na Gladnes mushi, arusha
picha na Gladnes mushi, arusha
Mbunge wa Arumeru Joshua Nasari akiwa amekaa na mjane wa marehemu Kiriro kushoto ambaye alikuwa mmeru wa kwanza kwenda kudai
uhuru akimpeleka kutoa sadaka shukrani mara baada ya kuchaguliwa kuwa
mmbunge.
Mbunge Joshua Nasari akitoa shukurani zake kanisani.
Gladness Mushi wa Full shwangwe -Arusha
Mbunge wa jimbo la
Arumeru Mashariki Bw Joshua Nassari leo amefanikiwa kutoa sadaka ya
shukurani katika kanisa la FPCT Kilinga wilayani meru mara baada ya
kuchaguliwa kama mbunge wa jimbo hilo
Akiongea na Mamia ya wananchi wa jimbo hilo
katika kanisa hilo
Bw Nassari alisema kuwa ameamua kutoa sadaka maalumu ya kushukuru mungu mara
baada ya kumaliza vema uchaguzi huku wapiga kura wake wote wakiwa salama
tofauti na pale ambapo wengi waliadhimia
hata ivyo aliwataka viongozi wa vyama vingine kuhakikisha kuwa
wanakuwa mstari wa mbele kutetea maslahui ny6a wananchi na kuachananna
tofauti za kivyama ambazo kama zitaendelezwa basi zitachangia kwa
kiwango kikubwa sana umaskini wa Meru
Akiongea katika kanisa hilo kwa ajili ya ibada hiyo mchungaji Langaeli Kahaya
naye alisema kuwa wananchi wanapswa kuhakikisha kuwa kamwe hawamchagui
kiongozi yoyote kwa ajili ya maslahi ya Rushwa kwa kuwa wote wanaotoa
rushwa ndio wanaosababisha hata umaskini
na umwagaji damu ndani ya nchi
Kutokana na hali hiyo alisema kuwa ni mwiko kwa wananchi wma
Jimbo la Arumeru Mashariki kujihusisha
na Rushwa kwa vipindi vyote vya uchaguzi kwa kuwa mpaka sasa Rushwa imeshaacha
madhara makubwa sana ndani ya jimbo hilo na pia Rushwa ni dhambi kubwa sana.
HABARI KWA HISANI YA FULLSHANGWE
No comments:
Post a Comment