Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, May 13, 2012

SIKU MOJA BAADA YA KUPOKELEWA KAMA MFALME ,KANISA LA ASKOFU KAKOBE LAMFANYIA MAOMBI MBUNGE FILIKUNJOMBE



SIKU moja baada ya mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kupokelewa jimboni na wapiga kura wake kama mfalme Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship(F.G.B.F) linaloongoza na askofu Zacharia Kakobe wilayani Ludewa lamfanyia maombi maalum .

Huku mwenyewe akiahidi kuendelea kupambana na Vitendo vya ufisadi kwa Taifa bila kuogopa na kuwaomba Waumini wa Kanisa hilo na madhehebu mengine pamoja na wapiga kura wake wote kuzidi kumwombea zaidi Kwani kazi iliyopo mbele yake ya kupambana na ufisadi ni nzito yahitaji maombi.

Kanisa hilo limfanyia mbunge Filikunjombe maombi hayo jana katika ibada maalum ambayo iliandaliwa na uongozi wa Kanisa hilo kama njia ya kuungana na vyama vya siasa na wananchi wa jimbo hilo kuutambua mchango na kazi nzito ya mbunge huyo katika kupambana na vitendo vya ufisadi nchini.

Katika maombi idaba hiyo Mchungaji wa Kanisa hilo Faustin Sambilanda.
alisema kuwa kazi ilinayofanywa na Filikunjombe katika kulipigania Taifa ni kubwa na hivyo kila mtanzania na kila kiongozi wa dini wanaowajibu wa kuendelea kumwombea mbunge huyo na wengine ambao wapo kwa maslahi ya watanzania .

No comments:

Post a Comment