Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, May 13, 2012

Angalia hapa wakali wa Kili Music Award 2012 walivyoiteka moshi




 Hadija Kopa na wasanii wa muziki wa Bongo fleva, Ali Kiba, Omy Dimpoz, Roma Mkatoliki AT, pamoja na wakali wa Ragge Warriors walikonga vilivyo nyoyo za mashabiki wa burudani mjini Moshi na kudhihirisha uhalali wao wa kutwaa Tuzo mbalimbali za Kili Music 2012. Zifuatazo ni picha mbalimbali za tukio hilo.

Pichani juuni Mkali wa Bongo Fleva, Ali Kiba akiimba jukwaani hii leo wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award iliyofanyika kwenye uwanja wa Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro  jana.


 Barnaba Boy ambaye ni mshindi wa Tuzo ya Mwimbaji Bora wa Kiume akimbo jukwaani hii leo wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award kwenye uwanja wa Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro  jana.


 Roma Mkatoliki akitumbuiza jukwaani wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award mkoani Kilimanjaro.


 DJ Choka akisugua vyombo kuendana na Roma Mkatoliki


 Hapa ni usiku ....


 ...ni mchana


 anastua...huyu ni Gwiji Hadija Kopa akifanya vitu vyake jukwaani hapo Ushirika. Mama alifunika mbaya katika show hii


 Wakali wa ragge kutoka kundi la Warriors from East la mjini Arusha wakitumbuiza mashabiki katika tamasha maalum la Washindi wa Kili Music Award 2012 kwenye uwanja wa Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro  jana.


 Msanii AT kutoka Zanzibar akitumbuiza jukwaani na wacheza show wake wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award kwenye uwanja wa Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro  jana.


 Hawa nao walikuwa wakitoa mpya ya kujirusha na kuangukia mgongo. Ni vijana wa Suma Lee.


 Suma Lee akifanya vitu vyake jukwaani



 Msanii anae kuja juu Omy Dimpoz nae akikamua jukwaani wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award mkoani Mwanza katika Uwanja wa Kirumba leo.


 Nai Nai hapa ikiimbwa maana Omy Dimpoz alimshirikisha Ali Kiba


 Wadau wakifuatilia show hiyo


Ali Kiba akienda sawa na vijana wake, hakika Moshi ilikuwa hapatoshi.

Gwiji la Muziki wa Taarabu nchini, na Mshindi wa Tuzo ya Mtumbuizaji bora wa Kike, Hadija Kopa akifanya makamuzi  katika tamasha maalum la Washindi wa Kili Music Award 2012 kwenye uwanja wa Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro  jana.
Mkali wa Bongo fleva Ali Kiba akiimba jukwaani hii leo wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award iliyofanyika kwenye uwanja wa Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro  jana.
Chipukizi wa Bongo Fleva, anaetambulika kwa jina la Sungura akitumbiza jukwaani, dogo huyu aliyeshinda katika shindano maalum la vipaji atakwenda jijini Dar es Salaam kurekodi wimbo wake kwa DJ mkali wa Bongo
 
 
GWIJI  la Taarab nchini Tanzania kutoka kundi la TOT, Hadija Omary Kopa na wasanii wa muziki wa Bongo fleva, Ali Kiba, Omy Dimpoz, Roma Mkatoliki AT, pamoja na wakali wa Ragge Warriors walikonga vilivyo nyoyo za mashabiki wa burudani mjini Moshi na kudhihirisha uhalali wao wa kutwaa Tuzo mbalimbali za Kili Music 2012.
Wasanii hao waliokuwa wakitumbuiza katika Tamasha maalum la Kili Music Award Winners Tour lililofanyika jana kwenye Uwanja wa Ushirika mjini hapa.
Licha ya hali ya hewa kuwa ya mvua na manyunyu ya hapa na pale wakati wote wa tamasha hilo lakini wakazi wa mji wa Moshi na vitongoji vyake jana walivunja rekodi ya Tamasha hilo kwa kujitokeza kwa wingi uwanjani hapo tofauti na mikoa mingine ya Dodoma na Mwanza ambako tayari Tanasha kama hilo limefanyika.
Kabla ya washindi wa Tuzo za Mziki za Kilimanjaro 2012 kupanda jukwaani walianza kupandaa chipoukuzi wa tatu wealio chuana vikali na mashabiki kumpitisha Msanii Sungura aliyeonekana kupagawisha vilivyo kwa wimbo wake wa Ndizi yangu.

Walianza jukwaani kupanda washindi wa Tuzo Bora ya Wimbo wa Ragge ambayo ilitwaliwa na kundi la Warriors from East waiotamba na vibao vyao kadhaa na kupiga jukwaani zaidi ya saa moja na kibao cha Arusha Gold kilichopawa tuzo kikiburudisha vilivyo na live show yao.
Mkongwe wa Taarab, Hadija Omary Kopa aliiudhihirishia umma wa wana Kilimanjaro kuwa yeye ni Mtumbuizaji bora wa Kike baada ya kupanda jukwaani na kuimba nyimbo zake kadhaa zilizojaa vijembe na mashairi ya ukweli ya taarab kutoka kundi lake la TOT huku uchezaji wake ukishangilia mwanzo hadi mwisho kwa jinsi alivyokuwa akiutikisa mwili wake.
  Mkali kutoka Zanzibar ambaye ni mshindi wa Tuzo Wimbo Bora wenye Vionjo vya Kiasili AT nae alipanda jukwaani nyuma ya Hadija Kopa na kutoa burudani ya nguvu na  wimbo wa  Vifuu Utundu amabao ulimpa tuzo aliucheza vilivyo na wanenguaji wake waili wa kike.
Akitanguliwa jukwaani na wacheza show wake machachari alikuwa ni mshindi wa Tuzo mbili za Kili Music Award 2012, Suma Lee aliyenyakua tuzo za wimbo bora wa Afro Pop kupiria kibao chake cha Hakunaga na Wimbo bora wa mwaka ambao pia ni hakunaga alikamua sawasawa.

No comments:

Post a Comment