Pages

Wednesday, May 23, 2012

UNAJUA NAKAAYA YUKO WAPI KWA SASA?SOMA HAPA

Nakaaya (Hii picha ilipigwa kabla ya kupata ajali).
Ni wengi wanajiuliza Nakaaya yuko wapi siku hizi, hajasikika kwenye nyimbo mpya wala kuzungumza chochote kwa kitambo.
sasa kwa  taarifa ni kwamba staa huyu wa single ya Mr Politician na nyingine kadhaa ametangaza kurudi kwenye muziki baada ya ukimya wa zaidi ya miezi sita.
Nakaaya amesema alipata ajali mbaya ya gari mwishoni mwa mwaka jana Arusha iliyomfanya alazwe hospitali kwa miezi minne huku mgongo na sura vikiwa vimeumia sana.
Hakuwahi kusema chochote kwenye media mpaka alipozungumza EXCLUSIVE  na millard ayo,  ambapo anakiri alipata wakati  mgumu sana na kuhisi kuchanganyikiwa pale alipoona kulikua na asilimia kubwa ya vitu alivyoshindwa kuvifanya kwa sababu ya ajali aliyopata.
Hakujihusisha na muziki kwa namna yeyote ile ila baada ya huo ukimya, sasa amerudi na amesema hataki kufocus kwenye chochote kingine zaidi ya muziki kwa sasa, anafanya project mpya na maproducer wakali kama Marco Chali & Lamar, nafanya mazoezi ya kutosha na yuko serious na muziki sasa hivi kwa sababu anauhakika kwa sasa unalipa vizuri.

No comments:

Post a Comment