Ni wengi wanajiuliza Nakaaya yuko wapi siku hizi, hajasikika kwenye nyimbo mpya wala kuzungumza chochote kwa kitambo.
sasa kwa
taarifa ni kwamba staa huyu wa single ya Mr Politician na nyingine kadhaa
ametangaza kurudi kwenye muziki baada ya ukimya wa zaidi ya miezi sita.
Nakaaya amesema alipata ajali
mbaya ya gari mwishoni mwa mwaka jana Arusha iliyomfanya alazwe
hospitali kwa miezi minne huku mgongo na sura vikiwa vimeumia sana.
Hakuwahi kusema chochote kwenye
media mpaka alipozungumza EXCLUSIVE na millard ayo, ambapo anakiri
alipata wakati mgumu sana na kuhisi kuchanganyikiwa pale alipoona
kulikua na asilimia kubwa ya vitu alivyoshindwa kuvifanya kwa sababu ya
ajali aliyopata.
Hakujihusisha na muziki kwa
namna yeyote ile ila baada ya huo ukimya, sasa amerudi na amesema hataki
kufocus kwenye chochote kingine zaidi ya muziki kwa sasa, anafanya
project mpya na maproducer wakali kama Marco Chali & Lamar, nafanya
mazoezi ya kutosha na yuko serious na muziki sasa hivi kwa sababu
anauhakika kwa sasa unalipa vizuri.
VODACOM YAFANYA MABORESHO MAKUBWA YA MTANDAO KUWAHAKIKISHIA WATEJA WAKE
HUDUMA BORA
-
Kampuni kinara ya teknolojia na mawasiliano nchini, Vodacom Tanzania,
imetangaza kufanya mabadiliko makubwa katika miundombinu ya mtandao wake
ikiwa ni ...
4 hours ago
No comments:
Post a Comment