Gerald Sanga akiwa hopitali baada ya kureruhiwa kwa risasi
WAKAZI WAWILI WAVAMIWA KWA RISASI IRINGA
Watu wawili kutoka katika sehemu tofauti na kwa nyakati tofauti katika Mkoa wa Iringa wamevamiwa na kupigwa na risasi watu wasiojulikana.
Akiongea
mmoja wa majeruhi hao aliyetambulika kwa jina la Gerald Sanga toka
Ifunda ameeleza kuwa usiku majira ya saa nane akiwa nyumbani alisikia
sauti ya mbwa akibweka na kujaribu kutoka nje ili kuangalia ndipo
alipopigwa na kudondoka chini huku watu hao waliotenda tukio hilo
kutokomea pasipo julikana.
Kwa
mujibu wa shuhuda wa tukio hilo aliyejulikana kama ibrahimu anaeleza
kuwa majeruhi huyo anaishi na bibi yake ambaye ni mfugaji wa ng’ombe na
kwa mujibu wa maelezo yake anasema kuwa uvamizi huo ulikuwa na lengo la
kuchukua fedha ambazo zimepatikana kutokana na uuzaji wa mifugo hiyo
lakini bila mafanikio walikimbia na kumjeruhi kijana huyo.
Katika
tukio jingine eneo la kinyika Pawaga katika mkoa wa IRINGA kijana
aliyetambulika kwa jina Isa Chatira(32) mfanyabiashara
anayejishughulisha na uuzaji wa mafuta alivamiwa na watu wasiojulikana
waliokuja kwa lengo la kununua mafuta.
Akizungumza
huku akiwa na maumivu makali Chatira amesema alikuwa kwake baada ya
kufunga biashara lakini walitokea wateja ambao walimtaka awauzie mafuta
Lakini kabla ya kuwahudumia walimpiga risasi eneo la tumboni na
kutokomea pasipo julikana.
Kwa
mujibu wa maelezo ya baba wa Isa, Athumani Chatira anaeleza kuwa mwanae
huyo ambaye ni mfanya biashara wa mafuta aina ya petrol alivamiwa na
watu wasiojulikana. Athumani amezidi kubainisha kuwa kwa mujibu wa Xray
iliyofanyika katika hospitali ya mkoa wa Iringa inaonesha kuwa hakuna
risasi iliyoingia lakini bado majeruhi yupo katika hali mbaya.
Bado mtandao unazidi kufuatilia habari hizi toka kwa maafisa usalama na madaktari ili kupata ukweli……..
No comments:
Post a Comment