Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, June 21, 2012

AFANDE SELE : NEY NDIO NANI, MAJINA HAYO NAJUA NI YA MADEM, SASA IWEJE NEEMA ANIDISS MIMI?



 
"Simjui huyo Ney ni nani anaigiza filamu au ni demu gani? mimi najua  majina kama hayo ni ya mademu sasa iweje Neema anidiss mimi?"
NI kauli ya  nyota mwenye 'Crown' ya mkali wa Rhymes nchini Seleman Msindi 'Afande Sele'  alipokuwa akizungumza na Teentz.com kuhusiana na 'diss' dhidi yake iliyotolewa na  msanii mwenye uwezo mkubwa wa kuchana hivi sasa hapa Bongo, Ney wa Mitego kupitia  track yake mpya  iliyopewa jina la 'Nasema  Nao'.
Akizungumza na mtandao huu namba moja ka habari za mastaa, Afande Sele mwenye maskani yake  pande za  Morogoro amesema kuwa kamwe hajawahi kusikia  wala kujua kama  kuna msanii wa hip hop hapa Bongo anayeitwa Ney na kusisisitiza kuwa hamjui huyo mtu kabisa.
Alipotakiwa kusema kama ameisikia Track hiyo Sele  alifunguka  kuwa  hajui kitu chochote kuhusu wimbo huo na anaamini kuwa hakuna wimbo wa  Hip hop ulitolewa hivi karibuni.
"Binafsi sijaisikia na sijui lolote,nitajaribu kufuatilia,nitaitafuta track hiyo niisikilize na kama atakuwa amefanya hivyo basi nitamlinganisha na mtu anayemtukana Usain Bolt halafu akaanza kukimbia  alisema Sele.

No comments:

Post a Comment