MSHAMBULIAJI
wa Dong Tam Long An ya Vietnam, Danny Davis Mrwanda amesaini mkataba wa
mwaka mmoja wa kuichezea Simba, ambao hauna kipengele cha kumruhusu
kuuvunja kabla haujamalizika.
Mrwanda (pichani kushoto),
awali ilielezwa anataka kusaini mkataba ambao wakati wowote akipata
timu nje, aondoke, lakini kwa mujibu wa mkataba aliosaini Simba ni
kwamba akipata timu italazimika kumnunua kutoka kwa Wekundu wa Msimbazi,
au isubiri hadi amalize mkataba.
Habari
za uhakika, kutoka ndani ya Simba SC ambazo, zimesema kwamba Mrwanda
ameridhika na mkataba huo na ameahidi kufanya vitu baab kubwa Msimbazi.
Kwa
upande mwingine, Simba SC imeamua kumtema kiungo Salum Machaku kwa
makubaliano maalum ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba. Simba ilitaka
kumtoa kwa mkopo Machaku, lakini mwenyewe akasema bora aachwe moja kwa
moja.
Tayari
Simba imemsajili kiungo wa Yanga, Kiggi Makassy kuziba nafasi ya
Machaku. Machaku sasa ameingia kwenye mazungumzo na Yanga.
No comments:
Post a Comment