Pages

Monday, June 18, 2012

MRWANDA ASAINI MWAKA MMOJA SIMBA SC


MSHAMBULIAJI wa Dong Tam Long An ya Vietnam, Danny Davis Mrwanda amesaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuichezea Simba, ambao hauna kipengele cha kumruhusu kuuvunja kabla haujamalizika.
Mrwanda (pichani kushoto), awali ilielezwa anataka kusaini mkataba ambao wakati wowote akipata timu nje, aondoke, lakini kwa mujibu wa mkataba aliosaini Simba ni kwamba akipata timu italazimika kumnunua kutoka kwa Wekundu wa Msimbazi, au isubiri hadi amalize mkataba.
Habari za uhakika, kutoka ndani ya Simba SC ambazo, zimesema kwamba Mrwanda ameridhika na mkataba huo na ameahidi kufanya vitu baab kubwa Msimbazi.
Kwa upande mwingine, Simba SC imeamua kumtema kiungo Salum Machaku kwa makubaliano maalum ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba. Simba ilitaka kumtoa kwa mkopo Machaku, lakini mwenyewe akasema bora aachwe moja kwa moja.
Tayari Simba imemsajili kiungo wa Yanga, Kiggi Makassy kuziba nafasi ya Machaku. Machaku sasa ameingia kwenye mazungumzo na Yanga.

No comments:

Post a Comment