Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, July 26, 2012

CHAMA CHA WALIMU CHAWAAGIZA WANACHAMA WAKE KUANZA KUPIGA KURA ZA KUKUBALI AU KUPINGA MGOMO.






Rais Chama cha Walimu nchini (CWT) Mwl. Gratian Mukoba akitoa taarifa ya chama hicho kuwataka wanachama wake kuanza kupiga kura za kukubali au kupinga mgomo ambapo pamoja na mambo mengine chama kimewaomba wanafunzi na wazazi watakaokuwa wameathirika na mgomo huo kuwavumilia waalimu kwa kuwa bila walimu kupata mishahara inayokidhi hali halisi ya maisha, utendaji wao wa kazi utaendelea kuathirika.
Pichani Juu na Chini ni baadhi ya walimu wakisikiliza taarifa iliyokuwa ikitolewa na Rais wa Chama cha Walimu Tanzania kuhusiana na suala la mgomo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakisikiliza taarifa ya Chama cha walimu Tanzania (CWT).
Na.MO BLOG TEAM
Chama cha Walimu Tanzania CWT kimeawaagiza wanachama wake kuanza kupiga kura baada ya kupewa Cheti cha kuonyesha kuwa usuluhishi umeshindikana.
Akizungumza na vyombo vya habari leo, Rais CWT Mwl. Gratian Mukoba amesema ikiwa waalimu watakaounga mkono mgomo watakuwa wengi kuliko wale watakaokuwa wamepinga mgomo, Baraza la Taifa la CWT litakutana kwa dharura kutangaza mgomo kwa kuwaelekeza wanachama wa CWT na serikali kuhusu aina ya mgomo ambao utakuwa umeamuliwa na muda wa mgomo.
Amefafanua kuwa ya kujadiliana kwa muda wa siku 30 kama sheria inavyoelekeza, siku 30 zilianza kuhesabiwa tangu Juni 26, 2012 na zimemalizika Julai 25 2012 kwa Msuluhishi aliyeteuliwa na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi Ndugu Cosmas Fimbo Msigwa kutoa Cheti cha Kuthibitisha kuwa mgogoro umeshindikana kusuluhishwa kwa mujibu wa Sheria.
Chama cha Walimu pia kimewajulisha wanachama wake na serikali kwa ujumla mgomo huo hauna uhusiano na Sensa ya Watu na Makazi.
                                         SOURCE http://networkedblogs.com

No comments:

Post a Comment