Rais
Chama cha Walimu nchini (CWT) Mwl. Gratian Mukoba akitoa taarifa ya
chama hicho kuwataka wanachama wake kuanza kupiga kura za kukubali au
kupinga mgomo ambapo pamoja na mambo mengine chama kimewaomba wanafunzi
na wazazi watakaokuwa wameathirika na mgomo huo kuwavumilia waalimu kwa
kuwa bila walimu kupata mishahara inayokidhi hali halisi ya maisha,
utendaji wao wa kazi utaendelea kuathirika.
Pichani
Juu na Chini ni baadhi ya walimu wakisikiliza taarifa iliyokuwa
ikitolewa na Rais wa Chama cha Walimu Tanzania kuhusiana na suala la
mgomo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakisikiliza taarifa ya Chama cha walimu Tanzania (CWT).
Na.MO BLOG TEAM
Chama
cha Walimu Tanzania CWT kimeawaagiza wanachama wake kuanza kupiga kura
baada ya kupewa Cheti cha kuonyesha kuwa usuluhishi umeshindikana.
Akizungumza
na vyombo vya habari leo, Rais CWT Mwl. Gratian Mukoba amesema ikiwa
waalimu watakaounga mkono mgomo watakuwa wengi kuliko wale watakaokuwa
wamepinga mgomo, Baraza la Taifa la CWT litakutana kwa dharura kutangaza
mgomo kwa kuwaelekeza wanachama wa CWT na serikali kuhusu aina ya mgomo
ambao utakuwa umeamuliwa na muda wa mgomo.
Amefafanua
kuwa ya kujadiliana kwa muda wa siku 30 kama sheria inavyoelekeza, siku
30 zilianza kuhesabiwa tangu Juni 26, 2012 na zimemalizika Julai 25
2012 kwa Msuluhishi aliyeteuliwa na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi Ndugu
Cosmas Fimbo Msigwa kutoa Cheti cha Kuthibitisha kuwa mgogoro
umeshindikana kusuluhishwa kwa mujibu wa Sheria.
Chama cha Walimu pia kimewajulisha wanachama wake na serikali kwa ujumla mgomo huo hauna uhusiano na Sensa ya Watu na Makazi.
SOURCE http://networkedblogs.com
No comments:
Post a Comment