NA GLADNESS MUSHI WA FULLSHANGWE-ARUSHA
MATUMIZI ya dawa za kurefusha maisha kwa watu wenye ugonjwa wa Ukimwi nchini ,ARVS,sanjari na elimu inayotolewa ya kupambana na maambukizi ya Ukimwi,yamepunguza idadi ya vifo vinavyotokana na Ugonjwa wa Ukimwi na kuwawezesha kushiriki katika shughuli zao za kujipatia vipato na kuongeza tija katika shughuli zao za kila siku .
Hayo yameelezwa na Daktari Twaha Ahmed, alipokuwa akitoa mada kwenye semina ya mafunzo elekezi kwa wanahabari kuhusu maambukizi yaVirusi vya ugonjwa wa Ukimwi na kueleza kuwa matumizi hayo yamekuwa na faida kubwa kwa wananchi ambao wameshaathirika na sasa wanaendelea kutumia dawa hizo za kurefusha maisha.

Dakta,
Twaha, ambae ni mshauri wa maswala ya afya ya binadamu katika mashirika
na taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa ,ametolea mfano wa nchi
ya Brazil ,barani Amerika ya kusini, kuwa ni ya mfano kutokana na
wananchi wake ambao wameathirika na Ukimwi wamekuwa wakitumia dawa hizo
za ARVS kwa ajili ya kurefusha maisha bila kuachia njiani na sasa
wanaendelea vizuri na wanashiriki katika shughuli za uzalishaji mali.
No comments:
Post a Comment