El
Salam Wau ya Sudan Kusini na Atletico ya Burundi zinatarajiwa kuwa timu
za kwanza kuwasili nchini kushiriki michuano ya Klabu Bingwa Afrika
Mashariki na Kati (Kombe la Kagame).
Michuano
hiyo inaanza kutimua vumbi Jumamosi (Julai 14 mwaka huu) kwenye Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam ikishirikisha timu kumi na moja akiwemo bingwa
mtetezi Yanga na makamu bingwa Simba.
Kikosi
cha El Salam Wau ambacho kitawasili kesho alfajiri (Julai 11 mwaka huu)
kwa ndege ya Ethiopia Airlines kikitokea Juba kupitia Addis Ababa,
Ethiopia kikiwa na wachezaji 18 na viongozi saba.
Wachezaji
wanaounda kikosi hicho ni Khamis Leone Uso Wani (nahodha), Adheil
Bugwic Jongkor Bugwic, Edward Joram Simon Julio, Fidel Andrea Fides Fas,
Ismael Musa Juma Ismael, James Anei Matheli Anei, Jervas Ayo Abdalla
Ayak, Khamis Doshama Ulama Andel na Meki Sultan Berema Kuku.
Wengine
ni Moga Emmanuel Androga, Mubarak Mohammed Saleh Omer, Ndili Rabeh
Nasir Hozi, Nizir Rihan Taban Talib, Oliver Paul Kangi Akok, Rabie
Mohammed Abubakar Hassan, Rufino Joseph Uras Ambros, Santino Makuei Uyu
Upio, Thomas Rufino Thomas Diakon.
Nayo
Atletico inatarajiwa kuwasili kesho (Julai 11 mwaka huu) kwa usafiri wa
barabara. Timu hiyo inakuja kwa usafiri wa basi lake ambalo pia
italitumia kwa muda wote itakapokuwa kwenye mashindano.
Wakati
El Salam Wau itafikia kwenye hoteli ya Rungwe iliyoko maeneo ya
Kariakoo, Atletico itakuwa Lunch Time Hotel iliyoko Mabibo.
Timu
zinazotarajiwa kuwasili keshokutwa (Julai 12 mwaka huu) ni Mafunzo ya
Zanzibar kwa boti saa 9 alasiri, Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya
Congo (RDC) itatua saa 1.20 usiku kwa Kenya Airways. Timu nyingine
itakayowasili siku hiyo jioni ni URA ya Uganda.
No comments:
Post a Comment