Pages

Thursday, July 5, 2012

MAOMBI YA MCHANGO KUFANIKISHA MALENGO YA SHEREHE YA MIAKA 100 YA HOSPITALI TEULE YA WILAYA YA KARAGWE



ELCT/KARAGWE DIOCESE
Kwa wadau wote wa Maendeleo
Mkoa wa Kagera
Yah: MAOMBI YA MCHANGO KUFANIKISHA MALENGO YA SHEREHE YA MIAKA 100 YA HOSPITALI TEULE YA WILAYA YA KARAGWE
 - NYAKAHANGA DDH
Somo hapo juu linahusika.
Hospitali tajwa inaadhimisha miaka 100 tangu kuanza kutoa huduma za tiba na afya katika wilaya ya Karagwe. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni: Shabaha Yetu ni Huduma Bora za Afya na Tiba
Maadhimisho hayo yatafanyika tangu tarehe 27 Agosti na kilele kuwa tarehe 2 Septemba. Katika wiki hii, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali  kutakuwa na maonyesho yatakayoenda sambamba na utoaji wa huduma za afya bure kwa wananchi watakotembelea mabanda yaliyoandaliwa.
Uchunguzi wa afya kama vile Kisukari, moyo, shinikizo la damu, upimaji wa VVU, uchunguzi wa saratani ya matiti kwa akina mama, huduma za macho na uzazi n.k zitatolewa kwa kushirikiana na wataalam wa ndani na nje ya nchi.

No comments:

Post a Comment