Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ally Iddi akimkabidhi vifaa
vya huduma na tiba, Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kata ya Kimara, Dk.
Alphoncina Mbinda katika hafla maalum iliyofanyika jana, kwenye Zahanati
hiyo, Kimara, Dar es Salaam. Vifaa hivyo vya sh. milioni 5.1,
vimepatikana kutokana na michango ya wanachama na viongozi wa Jumuia ya
Wazazi Tanzania. Wengine katika picha ni baadhi ya viongozi wa Jumuia ya
Wazazi, Katibu Mkuu Hamis Dadi (kulia) Katibu Wilaya ya Kinondoni,
Stanley Mkandawile (wapili kulia), na katikati ya Makamu na Mganga
Mfawidhi ni Kaimu Mwenyekiti wa Jumuia hiyo, Dogo Mabrouk. |
No comments:
Post a Comment