Pages

Thursday, July 5, 2012

HUYU NDIO MWIMBAJI ALIEKUBALI HADHARANI KWAMBA YEYE NI SHOGA.



.
Kwa Afrika ni uamuzi mgumu sana kufikia kukubali tena hadharani kwamba uko kwenye uhusiano wa kimapenzi wa jinsia moja, lakini kwa nchi nyingine zilizoendelea sio kitu kigumu sana.
Ni uamuzi mgumu pamoja na kwamba tumeona mataifa makubwa yakiunga mkono ushoga pamoja na watu maarufu kama mmoja wa maboss wa mtandao wa Facebook Chris Hughes kumuoa mwanaume mwenzake, Rais Obama wa Marekani, Jay Z na watu wengine pia wameonyesha msimamo wao kwamba hawana tatizo na ndoa za jinsia moja.
Baada ya kukupa Intro yote hiyo hapo juu stori kamili ni kwamba Staa wa muziki wa RNB kutoka Marekani Frank Ocean (24) amekubali hadharani kwamba yeye ni shoga, yani amekua akishiriki mapenzi ya jinsia moja.
Haya yote yamefahamika baada ya Ocean kuamua kuandika barua kuhusu ishu yake ya kushiriki mapenzi ya jinsia moja baada ya fununu kusikika kwa muda mrefu ambapo amesema alipokua na umri wa miaka 19 ndio alifall inlove kwa mwanaume aliependa anavyosmile pamoja na mambo mengine yaliyomvutia, Kwenye album yake mpya pia kuna baadhi ya mistari inayomsifia mwanaume kimapenz katika nyimbo zisizopungua tatu.
Hiyo hapo chini ni video ya moja kati ya nyimbo zake, unaweza kuitazama kama ulikua humfahamu…

No comments:

Post a Comment