skip to main |
skip to sidebar
HUYU NDIO MWIMBAJI ALIEKUBALI HADHARANI KWAMBA YEYE NI SHOGA.
.
Kwa Afrika ni uamuzi mgumu sana
kufikia kukubali tena hadharani kwamba uko kwenye uhusiano wa kimapenzi
wa jinsia moja, lakini kwa nchi nyingine zilizoendelea sio kitu kigumu
sana.
Ni uamuzi mgumu pamoja na
kwamba tumeona mataifa makubwa yakiunga mkono ushoga pamoja na watu
maarufu kama mmoja wa maboss wa mtandao wa Facebook Chris Hughes
kumuoa mwanaume mwenzake, Rais Obama wa Marekani, Jay Z na watu wengine
pia wameonyesha msimamo wao kwamba hawana tatizo na ndoa za jinsia
moja.
Baada ya kukupa Intro yote hiyo
hapo juu stori kamili ni kwamba Staa wa muziki wa RNB kutoka Marekani
Frank Ocean (24) amekubali hadharani kwamba yeye ni shoga, yani amekua
akishiriki mapenzi ya jinsia moja.
Haya yote yamefahamika baada ya
Ocean kuamua kuandika barua kuhusu ishu yake ya kushiriki mapenzi ya
jinsia moja baada ya fununu kusikika kwa muda mrefu ambapo amesema
alipokua na umri wa miaka 19 ndio alifall inlove kwa mwanaume aliependa
anavyosmile pamoja na mambo mengine yaliyomvutia, Kwenye album yake mpya pia kuna baadhi ya mistari inayomsifia mwanaume kimapenz katika nyimbo zisizopungua tatu.
Hiyo hapo chini ni video ya moja kati ya nyimbo zake, unaweza kuitazama kama ulikua humfahamu…
No comments:
Post a Comment