Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, July 29, 2012

MADIWANI MWANZA WAMNG'OA MEYA WA HALMASHAURI YA JIJI, WAPIGA KURA YA KUTOKUA NA IMANI NAYE



Na  Mashaka Baltazar wa Fullshangwe-MWANZA
*Kura 28 zamng'oa ,wanane wataka abaki
AlLIYEKUWA Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza,Bw.Josephat Manyerere ameng’olewa katika nafasi hiyo jana baada ya kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye na  Madiwani,wakimtuhumu kutumia wadhifa wake vibaya,kushiriki vitendo vya rushwa na kushindwa kufanya kazi.

Tuhuma zingine dhidi ya Diwani huyo wa Kata ya Nyakato (CHADEMA) ni mwenendo mbaya wa ukosefu wa adabu ulemavu wa kimwili au kiakili kiasi cha kumfanya ashindwe kutekeleza majkumu yake kama mwenyekiti wa vikao vya halmashauri ya jiji.

Kutokana na kadhia hiyo, Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Bw.Wilson Kabwe, aliwasilisha hoja  ya Madiwani waliojiorodhesha na kufikia theluthi mbili ya wajumbe wapatao 17 kati ya wajumbe 33 wa vikao halali vya baraza la madiwani wa Jiji hilo,alidai suala hilo ni la kisheria na kanuni ya 80 za kudumu za halmashauri hiyo.

“Halmashauri inaweza kumuondoa Mwenyekiti au Meya madarakani kwa azimio linaloungwa mkono na theluthi mbili ya wajumbe kutokana na sababu yoyote ya  ni (a) Kutumia nafasi yake vibaya(b),Kushiriki vitendo vya rushwa(c),Kushindwa kazi(d),Mwenendo mbaya wa ukosefu wa adabu na(e) ulemavu wa kimwili aidha kiakili kwa kiasi cha kumfanya kushindwa kutekeleza majukumu yake kama Mwenyekiti ama Meya.” Alifanunua Kabwe.

Tuhuma hizo kumi zilizowasilishwa kwa wajumbe na kusababisha kung’olewa kwake zilitajwa kwanza ni pamoja na kusimamia ujenzi wa kanisa moja bila kufuata utaratibu na kanuni za Halmashauri,kutoa maelezo kwa barua ya kushinikiza madiwani wenzake kuihoji na kupinga bajeti ambayo kimsingi na kikanuni bajeti hiyo niya kwakwe pia na ndiye msimamizi akiwa Meya.

No comments:

Post a Comment