Na Mashaka Baltazar wa Fullshangwe-MWANZA
*Kura 28 zamng'oa ,wanane wataka abaki
AlLIYEKUWA
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza,Bw.Josephat Manyerere
ameng’olewa katika nafasi hiyo jana baada ya kupigiwa kura ya kutokuwa na imani
naye na Madiwani,wakimtuhumu kutumia
wadhifa wake vibaya,kushiriki vitendo vya rushwa na kushindwa kufanya kazi.
Tuhuma
zingine dhidi ya Diwani huyo wa Kata ya Nyakato (CHADEMA) ni mwenendo mbaya wa
ukosefu wa adabu ulemavu wa kimwili au kiakili kiasi cha kumfanya ashindwe
kutekeleza majkumu yake kama mwenyekiti wa
vikao vya halmashauri ya jiji.
Kutokana na kadhia hiyo,
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Bw.Wilson Kabwe, aliwasilisha hoja ya Madiwani waliojiorodhesha na kufikia
theluthi mbili ya wajumbe wapatao 17 kati ya wajumbe 33 wa vikao halali vya
baraza la madiwani wa Jiji hilo,alidai suala hilo ni la kisheria na kanuni ya
80 za kudumu za halmashauri hiyo.
“Halmashauri inaweza
kumuondoa Mwenyekiti au Meya madarakani kwa azimio linaloungwa mkono na
theluthi mbili ya wajumbe kutokana na sababu yoyote ya ni (a) Kutumia nafasi yake
vibaya(b),Kushiriki vitendo vya rushwa(c),Kushindwa kazi(d),Mwenendo mbaya wa
ukosefu wa adabu na(e) ulemavu wa kimwili aidha kiakili kwa kiasi cha kumfanya
kushindwa kutekeleza majukumu yake kama Mwenyekiti ama Meya.” Alifanunua Kabwe.
Tuhuma hizo kumi
zilizowasilishwa kwa wajumbe na kusababisha kung’olewa kwake zilitajwa kwanza
ni pamoja na kusimamia ujenzi wa kanisa moja bila kufuata utaratibu na kanuni
za Halmashauri,kutoa maelezo kwa barua ya kushinikiza madiwani wenzake kuihoji
na kupinga bajeti ambayo kimsingi na kikanuni bajeti hiyo niya kwakwe pia na
ndiye msimamizi akiwa Meya.
No comments:
Post a Comment