Na Joseph 'Josefly' Muhozi
Mhadhiri
(lecturer) wa chuo kikuu cha Mtakatifu Augustino ama SAUT, Mwanza,
ameguswa na mashairi ya ngoma ya Fareed Kubanda a.k.a Fid Q yaliyopo
kwenye ngoma yake MWANZA MWANZA.
Denis
Mpagaze, mtaalam wa masomo ya journalism and communication research,
mwandishi wa vitabu na journals mbalimbali na mjuzi wa mambo ya falsafa,
amewashangaza wanafunzi wake ambao wamezoea kukuta matangazo mbalimbali
kwenye page yake ya facebook yanayohusu masomo na quotation za
waandishi maarufu wa vitabu.
Tofauti
na siku zote, wanafunzi wake wamekutana na maandishi yanayosema,
“‘‘USIJARIBU KUPIMA KWA SHINGO UKALI WA UPANGA AU KUIMBA UNAKULA KARANGA
NA SUMU KWA KUILAMBA...MANENO NI MKUKI, HEKIMA NGAO... (FID Q)
Kitendo
cha mhadhiri huyo kukubali uandishi wa Fid Q, unadhihirisha jinsi
mashairi yake yalivyotukuka, hata ukizima beat na snare bado maneno
anayotumia yanaweza kupenya na kugusa vichwa kama hivi katika vyuo
vikuu.
Mwenyewe Fid Q aliwahi kusema, ‘nasikika hata ukini-mute.’
Kutokana
na status ya mhadhiri huyo, maswali kibao yalizuka, “Kumbe unapenda
mistari ya wana hip hop sir? Aliuliza dada mmoja anaeitwa Neema Nyange.
Na
mwingine aitwaye Deogratias Konyani alisema, ‘Dah! Falsafa za
kitaaolojia by Fid Q! Hip hop unaipenda sir?’ huku Maulid Mombo naye
akiungana na wenzie kuuliza,’Dah ticha umenifurahisha kumbe na we umo
safi bt umesikia kitu kipya cha fid q-Sihitaji rafiki ?’ na Garma Paul
kuchangia, ‘ticha we mwana hip hop nini?’
Kutoka
na maswali hayo, mhadhiri huyo akajibu kwa kusema, ‘Namaanisha
kimaisha, kwenye fani ukiwa na akili unatoka vizuri sana na haraka,
kwenye vitabu hata uwe committed kiasi gani unakuja kutoka uzeeni’
Does
this mean huyu mwalimu anatamani kuingia kwenye game ili afikishe
alichoandika kwenye vitabu kwa wahusika haraka zaidi? I can’t tell, ila
alikili kuwa anayo album ya Fid Q tayari mkononi na ili kudhihirisha
kuwa anayajua mashairi kibao ya NGOSHA aliandika, ‘Akupigaye ngumi ya
jicho na we mpige ya sikio, akikuuliza unaonaje na we muulize
unajiskiaje.....ni vigumu majivu kuwa mkaa..’
No comments:
Post a Comment