Macho yote leo ni huko London, Uingereza kwenye sherehe za ufunguzi wa mashindano ya Olimpiki 2012.
Ufunguzi huo wa saa tatu ulioandaliwa na mshindi wa tuzo za Oscar muongozaji wa filamu ya Slumdog Millionaire, Danny Boyle utaangaliwa na watu 60,000 kwenye uwanja maalum wa mashindano hayo uliojengwa huko East End, London na kuangaliwa kwenye runinga na watazamaji zaidi ya bilioni moja duniani kote.
Sherehe hizo zitarushwa kuanzia saa 3 usiku kwa saa za huko ambayo ni sawa na saa sita usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Watazamaji watatakiwa kuimba pamoja na watumbuizaji na kutengeneza picha ya aina yake kwenye tukio hilo kubwa kabisa litakalokaribisha wanamichezo 16,000 kutoka nchini 204 duniani.
Kutakuwa na ulinzi mkali kwenye mashindano hayo unaotolewa na kampuni ya ulinzi y G4S.
Mamlaka zinazohusika na kukabiliana na ugaidi zimesema hakuna wasiwasi wa matukio hayo huku waziri mkuu wa Uingereza David Cameron akisema Olimpiki yenye usalama kilikuwa ni kipaumbele chake.
No comments:
Post a Comment