THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA YA SERIKALI KUHUSU KUSUDIO LA WALIMU KUGOMA
____________________________________________
SERIKALI
kupitia Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi leo, Ijumaa, Julai 27, 2012
majira ya saa tisa alasiri, imepokea notisi ya saa arobaini na nane (48)
ya kusudio la walimu wanachama wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT)
kugoma kuanzia Jumatatu tarehe 30 Julai 2012 saa moja na nusu asubuhi.
Kabla
ya notisi hii kutolewa, Serikali imekuwa ikifanya jitihada nyingi za
kujadiliana na viongozi wa CWT kuhusu jinsi ya kuboresha maslahi ya
walimu kwa nia ya kumaliza suala hili kwa maelewano kwa kutumia vyombo
na ngazi mbali mbali za kisheria.
Kwa
sasa, shauri hili liko Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi na leo hii siku
ya Ijumaa tarehe 27 Julai, 2012 majira ya saa sita mchana pande zote
mbili zilifika Mahakamani, na Mahakama ikaamuru kwamba pande zote
zikamilishe maelezo yao ifikapo siku ya Jumanne tarehe 31 Julai, 2012
saa sita mchana, ili kuiwezesha Mahakama kuendelea kusikiliza shauri
hilo na hatimaye kutoa uamuzi.
Kwa hiyo, Mgomo huu siyo halali kwa sababu shauri hili bado liko Mahakamani.
Kwa
msingi huo hatua ya CWT kutoa notisi ya kuanza kwa mgomo kabla ya
kukamilika kwa shauri hili ni kukiuka taratibu halali za Kimahakama
ambazo kila mmoja anawajibika kuziheshimu.
Serikali
inapenda kuwafahamisha walimu wote kuwa kujihusisha na mgomo huu ni
kwenda kinyume cha Sheria, Kanuni na Taratibu za kazi. Hivyo, walimu
wanapaswa kupima madhara ya mgomo huu usiokuwa halali na Serikali
inawataka walimu kupuuza mgomo huo na kutokujihusisha nao. Walimu wote
wanatakiwa waendelee na kazi kama kawaida.
Peniel M. Lyimo
KAIMU KATIBU MKUU KIONGOZI
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
27 Julai, 2012
No comments:
Post a Comment