Pages

Thursday, July 5, 2012

NHC YASAINI MIKATABA YA BILIONI 165/- NA MABENKI KWA AJILI YA MIRADI YA UJENZI WA NYUMBA



Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu.

Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limesaini mikataba ya mkopo wa Sh bilioni 165 kutoka kwa taasisi tisa za fedha kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa miradi ya ujenzi wa nyumba pamoja na ununuzi wa ardhi ya akiba.

Hafla ya kusaini mkataba huo ilifanyika leo Dar es Salaam baina ya shirika hilo  na wakurugenzi wakuu wa taasisi hizo ambapo hali hiyo ilielezwa kuwa moja ya hatua zinazofanywa na NHC katika kutafuta mitaji kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi. 

Taasisi za fedha zilizotoa  mkopo huo pamoja na kiwango walichotoa kwenye mabano ni pamoja na CRDB (Sh bilioni 35), ECO Bank (Sh bilioni 2), TIB (Sh bilioni 22), BancABC  (Sh bilioni 4.2), NMB (Sh bilioni 26), CBA (Sh bilioni 24), LAPF (Sh bilioni  15), Azania (Sh bilioni saba) na Shelter Afrique (Sh bilioni 23).

No comments:

Post a Comment