Pages

Tuesday, July 10, 2012

PICHA MBALIMBALI ZA MECHI KATI YA YANGA NA JKT NA BIN ZUBEIRY




Wakipongezana baada ya bao la pili; kulia Hamisi Kiiza, Cannavaro na Niyonzima wamekumbatiana na Rashid Gumbo anayeondoka kushoto

KOCHA Mbelgiji Thom Saintfiet leo ameanza kazi vizuri Yanga, baada ya kuiongoza timu kushinda mabao 2-0 dhidi ya JKT Ruvu katika mchezo wa kirafiki jioni hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mabao ya Yanga yalifungwa na beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ dakika ya 18 kwa kichwa akiunganisha kona ya Juma Abdul, wakati la pili lilifungwa na Mwanasoka Bora wa Uganda, Hamisi Kiiza ‘Diego’ dakika ya 72, akiunganisha pasi ya nyota wa Rwanda, Haruna Niyonzima.
Katika mchezo wa leo, ilishuhudiwa mabadiliko ya kiuchezaji kwenye kikosi cha Yanga, wakicheza soka ya utulivu, bila kukimbia ovyo kama ilivyo ada yao, muda mwingi wakitulia kwenye eneo lao na kufanya mashambulizi ya mipango.
Yanga ilitumia mshambuliaji mmoja tu kwenye mchezo wa leo, Jerry Tegete huku viungo zaidi wakilundikwa uwanjani.
Baada ya mchezo huo, Thom alisema kwamba ameridhishwa na uchezaji wa timu na matokeo pia na anaamini taratibu timu itazidi kuimarika hadi kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
Alisema baada ya mechi ya leo, atakuwa na vipindi vitatu zaidi vya mazoezi kabla ya mechi ya ufunguzi wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame Jumamosi dhidi ya Atletico ya Burundi.
Alisema atafanya siku moja moja kuanzia kesho hadi Ijumaa kabla ya kushusha timu uwanjani Jumamosi kukata utepe wa Kagame. Yanga ndio mabingwa watetezi wa michuano hiyo, inayoshirikisha timu za Simba na Azam pia katika orodha ya wenyeji.    
Nizar anatia krosi

Kona langoni kwa JKT

Kona langoni kwa JKT

Cannavaro anampongeza Kiiza kupiga la pili

Mapumziko; Athumani Iddi 'Chuji' anaongoza timu kutoka uwanjani

Niyonzima akimkumbatia Kiiza kwa kuitumia vema pasi yake

Shangwe za bao zimeisha vijana wanarudi kazini

Yaw Berko baada ya kudaka bila kuruhusu nyavu zake kutikiswa, anakula muziki baada ya mechi

Mtakatifu Thom anampongeza Nahodha Cannavaro kwa kuwaongoxa vijana vizuri

Anawapojngeza na marefa pia kwa kuchezesha vizuri

Hatari langoni kwa JKT

Mapumziko; Mtakatifu Thom na vijana wake wanaelekea chumbani kubadilishana mawazo kabla ya ngwe ya pili

Hatari langoni kwa JKT

Baada ya mapumziko, Niyonzima akimuelekeza Kiiza wakati wanaelekea uwanjani. Kiiza aliingia kipindi cha pili

Tegete anafumua shuti, lakini Shaabn Dihile alidaka

Hatari tena langoni kwa JKT

Said Bahanuzi anachele

No comments:

Post a Comment