|
Wakipongezana
baada ya bao la pili; kulia Hamisi Kiiza, Cannavaro na Niyonzima
wamekumbatiana na Rashid Gumbo anayeondoka kushoto |
KOCHA
Mbelgiji Thom Saintfiet leo ameanza kazi vizuri Yanga, baada ya
kuiongoza timu kushinda mabao 2-0 dhidi ya JKT Ruvu katika mchezo wa
kirafiki jioni hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mabao
ya Yanga yalifungwa na beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ dakika ya 18 kwa
kichwa akiunganisha kona ya Juma Abdul, wakati la pili lilifungwa na
Mwanasoka Bora wa Uganda, Hamisi Kiiza ‘Diego’ dakika ya 72,
akiunganisha pasi ya nyota wa Rwanda, Haruna Niyonzima.
Katika
mchezo wa leo, ilishuhudiwa mabadiliko ya kiuchezaji kwenye kikosi cha
Yanga, wakicheza soka ya utulivu, bila kukimbia ovyo kama ilivyo ada
yao, muda mwingi wakitulia kwenye eneo lao na kufanya mashambulizi ya
mipango.
Yanga ilitumia mshambuliaji mmoja tu kwenye mchezo wa leo, Jerry Tegete huku viungo zaidi wakilundikwa uwanjani.
Baada
ya mchezo huo, Thom alisema kwamba ameridhishwa na uchezaji wa timu na
matokeo pia na anaamini taratibu timu itazidi kuimarika hadi kwenye
michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
Alisema
baada ya mechi ya leo, atakuwa na vipindi vitatu zaidi vya mazoezi
kabla ya mechi ya ufunguzi wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati,
Kombe la Kagame Jumamosi dhidi ya Atletico ya Burundi.
Alisema
atafanya siku moja moja kuanzia kesho hadi Ijumaa kabla ya kushusha
timu uwanjani Jumamosi kukata utepe wa Kagame. Yanga ndio mabingwa
watetezi wa michuano hiyo, inayoshirikisha timu za Simba na Azam pia
katika orodha ya wenyeji.
|
Nizar anatia krosi |
|
Kona langoni kwa JKT |
|
Kona langoni kwa JKT |
|
Cannavaro anampongeza Kiiza kupiga la pili |
|
Mapumziko; Athumani Iddi 'Chuji' anaongoza timu kutoka uwanjani |
|
Niyonzima akimkumbatia Kiiza kwa kuitumia vema pasi yake |
|
Shangwe za bao zimeisha vijana wanarudi kazini |
|
Yaw Berko baada ya kudaka bila kuruhusu nyavu zake kutikiswa, anakula muziki baada ya mechi |
|
Mtakatifu Thom anampongeza Nahodha Cannavaro kwa kuwaongoxa vijana vizuri |
|
Anawapojngeza na marefa pia kwa kuchezesha vizuri |
|
Hatari langoni kwa JKT |
|
Mapumziko; Mtakatifu Thom na vijana wake wanaelekea chumbani kubadilishana mawazo kabla ya ngwe ya pili |
|
Hatari langoni kwa JKT |
|
Baada ya mapumziko, Niyonzima akimuelekeza Kiiza wakati wanaelekea uwanjani. Kiiza aliingia kipindi cha pili |
|
Tegete anafumua shuti, lakini Shaabn Dihile alidaka |
|
Hatari tena langoni kwa JKT |
|
Said Bahanuzi anachele |
No comments:
Post a Comment