July 10, 2012
Millard Ayo na Jose Chameleone kwenye interview.Kwa
mara ya kwanza toka Show ya AMPLIFAYA ianzishwe zaidi ya siku 500
zilizopita, leo ndio interview ya kwanza na staa wa Afrika Mashariki
Jose Chemeleone kutoka area 256 imesikika akiwa na Millard Ayo.
Utazisikia Stori zake nyingi tu kwenye mfululizo wa show za AMPLIFAYA on
super brand Clouds fm na hapa millardayo.com!!! kuhusu muziki wake
najua hizo stori utakua umezisikia sana kwengine…. Ninachokifanya ni
kwenda deep zaidi kwenye maisha yake, Navifata vyote vilivyotokana na
jina lake. Huu ni mwaka wake wa 12 toka ameanza kuwa maarufu kwenye
muziki, Jose Chameleone anaetajwa kuwa kwenye list ya wanamuziki watano
matajiri wa muziki wa sasa Afrika Mashariki, leo amekubali macho yako
yasome vitu atakavyovitaja vinavyompa pesa nyingi tofauti na muziki kwa
sasa.
Hii ndio simu inaitwa CHEMELEONE ambayo inauzwa kwenye maduka mbalimbali Uganda, unaweza kuwaka line yoyote ya mtandao wa simu.
Amesema Moja kati ya ishu
anazopiga ni “kununua nyumba na kuziuza, kukodisha, pia kununua mashamba
na kuyauza huko Uganda, na kuna biashara nyingine nimeianza juzi juzi
ya CHAMELEONE MOBILE, nilikwenda China na kuungana na kampuni moja ya
China wakatengeneza simu inaitwa CHAMELEONE, hiyo ni moja kati ya kazi
zangu kubwa… watu wanazinunua sana nyumbani Uganda, ni handset ambayo
unaweza kuweka line ya mtandao wowote”
Kwenye line ya mwisho
ChameleonE kasema “hii ni kujaribu kufikiria nje ya box pamoja na
kujaribu kufanya mipango uliyokua nayo kichwani, na bado naendelea baada
ya hizo simu nataka kutengeneza vitu vingi zaidi.. nataka jamii yangu
inikumbuke kwa nilichowafanyia”
Hayo ndio aliyoyasema Staa wa
muziki Jose Chameleone wa Uganda nchi inayotajwa kuwa na wasanii
wanaoongoza kwa kuwa na pesa nyingi kuliko nchi yeyote Afrika Mashariki.
Tayari mpaka sasa kuna baadhi
ya mastaa ambao wamejaribu kupiga dealz nyingine mbali na muziki akiwemo
Lady JayDee ambae anamiliki Mgahawa, Jua Cali wa Kenya alitangaza
kuanza kutengeneza headphone kama za Beat by Dre, Profesa Jay nae
alitangaza kwamba ndoto zake hazipo kwenye magari ya kifahari sasa hivi
au anasa nyingine, anajipanga kwa ajili ya kuinvest kwenye ardhi for
No comments:
Post a Comment