Temeke
imekuwa timu ya kwanza kupata tiketi ya kucheza nusu fainali kwenye
michuano ya mwaka huu ya Copa Coca-Cola baada ya kuing’oa Mjini
Magharibi kwa mikwaju ya penalti.
Mechi
hiyo ya kwanza ya robo fainali imechezwa leo asubuhi (Julai 10 mwaka
huu) Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam ambapo hadi dakika 90
za kawaida zinamalizika timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1.
Mjini
Magharibi ndiyo walioanza kupata bao dakika ya 79 lililofungwa na Salum
Maulid wakati Abdul Hassan aliisawazishia Temeke dakika ya 90.
Waliofunga
penalti kwa upande wa Temeke ni Baraka Ntalukundo, Khalid Mwendakamo,
Mohamed Dikougwa na Abdul Hassan wakati aliyekosa ni Anwar Kilemile.
Waliokosa kwa Mjini Magharibi ni Abdulrahman Mohamed na Salum Maulid
wakati waliofunga ni Alawi Kombo na Salum Shukuru.
Katika
nusu fainali, Temeke itacheza na mshindi wa mechi ya robo fainali kati
ya Kinondoni na Mwanza itakayochezwa kesho asubuhi (Julai 11 mwaka huu)
Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Robo
fainali ya pili ya michuano hiyo kati ya Mara na Morogoro ilitarajiwa
kuchezwa leo jioni kwenye uwanja huo huo. Mechi nyingine ya robo fainali
itakayowakutanisha Dodoma na Tanga itachezwa kesho jioni.
No comments:
Post a Comment