Mara
kadhaa watoto mapacha wanapozaliwa wakiwa wameungana huwa inakua kazi
nzito kuwatenganisha na wakati mwingine huwa wanafariki wakiwa kwenye
zoezi la kutenganishwa na wengine wanapoteza maisha kutokana na pesa ya
hayo matibabu ya gharama kukosekana lakini kwa Malaysia wamepata bahati
wakati huu.
Kuna
watoto walizaliwa April 2011 wakiwa mapacha walioungana mguuni ambapo
baada ya juhudi za Madaktari mabingwa kufanya upasuaji, wamefanikiwa
kuwatenganisha hawa malaika Muaiman na Muaimin na wakabaki kuwa hai.
Idadi
kubwa ya wananchi wakiwemo wazazi waliokua wanaifatilia habari ya
watoto hawa wamejawa na furaha baada ya kusikia hilo zoezi limefanikiwa.
Pamoja
na kwamba upasuaji umefanikiwa, ugumu ulikuwepo kwenye sehemu ya
kuhifadhia mkojo mwilini ambayo pia ilikua imeungana toka wamezaliwa,
sasa hivi wapo chini ya uangalizi wa kitaalam mpaka hali yao itakapo
ruhusu kuruhusiwa kwenda nyumbani kwa mujibu wa Star news paper.
No comments:
Post a Comment