Raila Odinga akiwa anampigia Prezzo kura na picha akaiweka kwenye page yake ya twitter yenye watu zaidi ya elfu 67.
Jaribu kufikiria kama ni wewe
ndio ungekua umeshiriki shindano la Big Brother Africa alafu ukapigiwa
kura na Waziri mkuu wa nchi yako tena kura ambayo ametangaza hadharani
ikiwa imebaki wiki moja tu game kumalizika.
Waziri mkuu wa Kenya Raila
Odinga amekua kiongozi wa juu wa nchi mimi kuona ushahidi wake wa
kumpigia kura mshiriki wa shindano la Big Brother Africa ambalo baadhi
ya viongozi wakuu wamenukuliwa kwenye vyombo vya habari kwamba
hawaliungi mkono.
Jumatatu July 30 2012 Raila
Odinga alikwenda kwenye page yake ya twitter iliyo verrified na kuandika
kwamba tayari amepiga kura yake kwa Prezzo ndani ya Big Brother kwa
kutuma sms.
Shindano la Big Brother
linatarajiwa kumalizika July 5 2012 ambayo ni jumapili ijayo, ambapo
mpaka sasa Prezzo ndio anaongoza kwa kupigiwa kura nyingi za swali
wanaloulizwa watu ni Mshiriki gani wanaetaka ashinde.. chek hapo chini.
Hizi
ni kura za July 31 2012 saa tisa kamili usiku wa kuamkia July 31,
Prezzo wa Kenya ndio anaongoza kama unavyoona hapo juu anafata Lady May
ni wa Namibia, Keagana ni wa South Africa, Kyle ni wa Uganda, Talia ni
wa Zambia na Wati ni wa Malawi.
SOURCE http://millardayo.com/
No comments:
Post a Comment