Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, July 27, 2012

Tuzo za mwanasoka bora wa mwaka 2012 Wazalendo Best footballer of the Year Awards yaja





KAMPUNI ya Wazalendo Bright Media kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ipo kwenye mchakato wa kumpata mwanasoka bora wa mwaka 2012.

Tuzo hizo zinajulikana kwa jina laWazalendo Best footballer of the Year Awards, ambapo washiriki wanaoingia kwenye kinyang’anyiro hihi ni  Watanzania ambao wanacheza soka kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Kwa upande wa wageni wanaocheza Tanzania watakuwa na tuzo yao maalum ya mwanasoka bora wa kulipwa, ambayo ipo kwenye orodha ya tuzo 11 zinazowaniwa na wanasoka.

 Tuzo hizo 11 ni pamoja na kipa, beki, kiungo, mshambuliaji, mchezaji anayechipukia, mchezaji mkongwe zaidi kwenye ligi, mchezaji bora wa kigeni, mwanasoka bora kwa wanawake, tuzo ya heshima katika maendeleo ya soka la wanawake,  tuzo ya heshima kwa wachezaji wa zamani pamoja na tuzo ya mwanasaisa aliyesaidia katika maendeleo ya michezo Afrika.

Madhumuni ya kuandaa tuzo hii ni kuongeza ushindani kwenye ligi ya Tanzania Bara, pamoja na timu za taifa jambo litakalofanya kila mchezaji kujituma zaidi kulingana na majukumu analiyonayo kwenye timu.

Ni imani yetu kwamba hatua hii itaongeza uwajibikaji na utelekezaji wa majukumu kwa moro pia itaongeza moyo wa uzalendo kwa wachezaji wa kitanzania kwenye timu za taifa.
Kwa kuanza, mchakato huu mashabiki wa soka waliopo ndani na nje ya Tanzania wataweza kupendekeza majina ya wale inaowaona wanaweza kuwa bora katika kipindi cha miezi 11. Yaani  kuanzia Januari Mosi hadi Novemba 30 mwaka huu, ambapo watachagua kupitia mitandao ya kijamii ambazo ni blogs, twitter na face book.

Kadhalika wanaweza kuchangua kupitia siku zao za mikononi kwa kutumia namba maalum ambayo tutaitangaza baadaye.

Baada ya mashabiki kupendekeza majina, kamati ambayo itaongozwa na wataalam kutoka chama cha makocha wa soka Tanzania (Tafca), wachezaji wa zamani, waandishi wa habari za michezo pamoja na wadau wengine wa soka itapitisha majina 40 kwa ajili ya kuingia kwenye hatua ya fainali ambayo itafanyika mwishoni mwa Desemba 2012 jijini Dar es Salaam, kwa kuzingatia vigezo vitakavyotangazwa baadaye.

Baada ya majina kutajwa na kamati, jukumu la kumchagua mwanasoka bora wa mwaka 2012, pamoja na nafaso nyingine itafanywa na makocha pamoja na manahodha wa timu za Ligi Kuu Tanzania Bara ambapo kila klabu inayoshiriki ligi hiyo itakuwa na kura mbili. Moja ya kocha mkuu na nyingine na nahodha.

Sababu za kuwatumia makocha wa ligi kuu pamoja na manahodha wao ni kutokana na ukaribu na kufahamiana zaidi kati ya mchezaji na mchezaji au kocha na mchezaji jambo ambalo kimsingi litaweza kutoa mshindi sahihi.

Tunachua nafasi hii kuwaomba mashabiki wa soka kuchangia kadri watakavyoweza ili kupata washindi sahihi. Mchakato unaanza Agosti mosi mwaka 2012 na mwisho wa kuchagua ni Novemba 30 mwaka 2012.
na full shangwe

No comments:

Post a Comment