KAMPUNI
ya Wazalendo Bright Media kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ipo
kwenye mchakato wa kumpata mwanasoka bora wa mwaka 2012.
Tuzo
hizo zinajulikana kwa jina laWazalendo Best footballer of the
Year Awards, ambapo washiriki wanaoingia kwenye kinyang’anyiro hihi ni
Watanzania ambao wanacheza soka kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Kwa
upande wa wageni wanaocheza Tanzania watakuwa na tuzo yao maalum ya
mwanasoka bora wa kulipwa, ambayo ipo kwenye orodha ya tuzo 11
zinazowaniwa na wanasoka.
Tuzo
hizo 11 ni pamoja na kipa, beki, kiungo, mshambuliaji, mchezaji
anayechipukia, mchezaji mkongwe zaidi kwenye ligi, mchezaji bora wa
kigeni, mwanasoka bora kwa wanawake, tuzo ya heshima katika maendeleo ya
soka la wanawake, tuzo ya heshima kwa wachezaji wa zamani pamoja na
tuzo ya mwanasaisa aliyesaidia katika maendeleo ya michezo Afrika.
Madhumuni
ya kuandaa tuzo hii ni kuongeza ushindani kwenye ligi ya Tanzania Bara,
pamoja na timu za taifa jambo litakalofanya kila mchezaji kujituma
zaidi kulingana na majukumu analiyonayo kwenye timu.
Ni
imani yetu kwamba hatua hii itaongeza uwajibikaji na utelekezaji wa
majukumu kwa moro pia itaongeza moyo wa uzalendo kwa wachezaji wa
kitanzania kwenye timu za taifa.
Kwa
kuanza, mchakato huu mashabiki wa soka waliopo ndani na nje ya Tanzania
wataweza kupendekeza majina ya wale inaowaona wanaweza kuwa bora katika
kipindi cha miezi 11. Yaani kuanzia Januari Mosi hadi Novemba 30 mwaka
huu, ambapo watachagua kupitia mitandao ya kijamii ambazo ni blogs,
twitter na face book.
Kadhalika wanaweza kuchangua kupitia siku zao za mikononi kwa kutumia namba maalum ambayo tutaitangaza baadaye.
Baada
ya mashabiki kupendekeza majina, kamati ambayo itaongozwa na wataalam
kutoka chama cha makocha wa soka Tanzania (Tafca), wachezaji wa zamani,
waandishi wa habari za michezo pamoja na wadau wengine wa soka
itapitisha majina 40 kwa ajili ya kuingia kwenye hatua ya fainali ambayo
itafanyika mwishoni mwa Desemba 2012 jijini Dar es Salaam, kwa
kuzingatia vigezo vitakavyotangazwa baadaye.
Baada
ya majina kutajwa na kamati, jukumu la kumchagua mwanasoka bora wa
mwaka 2012, pamoja na nafaso nyingine itafanywa na makocha pamoja na
manahodha wa timu za Ligi Kuu Tanzania Bara ambapo kila klabu
inayoshiriki ligi hiyo itakuwa na kura mbili. Moja ya kocha mkuu na
nyingine na nahodha.
Sababu
za kuwatumia makocha wa ligi kuu pamoja na manahodha wao ni kutokana na
ukaribu na kufahamiana zaidi kati ya mchezaji na mchezaji au kocha na
mchezaji jambo ambalo kimsingi litaweza kutoa mshindi sahihi.
Tunachua
nafasi hii kuwaomba mashabiki wa soka kuchangia kadri watakavyoweza ili
kupata washindi sahihi. Mchakato unaanza Agosti mosi mwaka 2012 na
mwisho wa kuchagua ni Novemba 30 mwaka 2012.
na full shangwe
No comments:
Post a Comment